Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia)
akikagua matofali ya kuchoma katika mradi wa ufyatuaji tofali za kuchoma katika
gereza la wilaya ya Mbozi alipotembelea hivi karibuni katika ziara yake ya kikazi Mkoani Songwe.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike
akikagua moja ya tanulu la matofali ya kuchoma katika mradi wa ufyatuaji tofali
za kuchoma katika Kambi ya Mkwajuni ,
Wilayani Songwe, leo Oktoba 8, 2019 alipotembelea katika ziara yake ya kikazi Mkoani Songwe.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike
akiwasili jana Oktoba 7, 2019 katika ziara yake ya kikazi Gereza Ngwala.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa(katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine
Kasike(wa pili toka kulia) alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo leo
Oktoba 8, 2019. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Songwe, Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Lyazeck Mwaseba. (Picha na Jeshi la Magereza)
Na Mwandishi wetu, Songwe;
KAMISHNA
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amewataka Wakuu wa magereza Tanzania
Bara kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo agizo la Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa jeshi hilo kote nchini kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa
waliopo magerezani.
Akizungumza Mkoani Songwe mara baada
ya kukagua miradi ya ufyatuaji wa matofali ya kuchoma na ujenzi wa nyumba za
maafisa na askari katika magereza ya Ileje, Mbozi, Ngwala na Kambi ya Mkwajuni
iliyopo Mkoani Songwe, Kamishna Jenerali
Kasike amesema ujenzi wa makazi za askari unaoendelea katika vituo mbalimbali nchini
ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli katika kutatua changamoto ya
makazi kwa watumishi wa Jeshi hilo.
"Mkakati wa utatuaji wa changamoto ya uhaba wa nyumba za
Maafisa na askari lazima utiliwe mkazo na kupewa kipaumbele katika kuwatumia
wafungwa waliopo magerezani katika suala
la ujenzi sambambamba na uzalishaji wa chakula chakutosha ili kuipunguzia
Serikali gharama za kuwahudumia wahalifu wote walipo magerezani, "
alisema Kamishna Jenerali Kasike.
Katika hatua nyingine, Kamishna
Jenerali Kasike ameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Songwe kwa kuanzisha ujenzi wa
Gereza jipya katika mji wa Mkwajuni ambao ni Makao Makuu ya Wilaya ya Songwe.
Kamishna Jenerali Kasike amesema
uwepo wa gereza hilo katika wilaya ya Songwe utasaidia katika kumaliza tatizo
la msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye gereza la wilaya ya Mbozi.
“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki hivyo nimpongeze sana Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kuwezesha kuanza kwa ujenzi wa Gereza hili kimsingi utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza Mbozi,” amesema Jenerali Kasike.
“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki hivyo nimpongeze sana Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kuwezesha kuanza kwa ujenzi wa Gereza hili kimsingi utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza Mbozi,” amesema Jenerali Kasike.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Songwe.
Mhe. Samwel Opulukwa ameshukru ujio wa Kamishna Jenerali katika ziara yake ya
kikazi katika Gereza la Ngwala pamoja na Kambi ya Mkwajuni ili kujionea hali
halisi ya Uendeshaji wa Jeshi hilo, Wilayani Songwe.
“Kamishna Jenerali
nikuhakikishie tu kuwa Uongozi wa wilaya utashirikiana na Jeshi la Magereza
katika kuhakikisha kuwa tunakamilisha ujenzi wa gereza hili jipya la Mkwajuni
ili kusaidia kuondoa usumbufu wa wahalifu kwenda gereza la wilaya ya mbozi,”
Alisistiza Mhe. Opulukwa.
Kwa sasa, wakazi wa wilaya hiyo ya Songwe ambao wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali au waliohukumiwa vifungo hupelekwa katika Gereza la wilaya ya Mbozi kitendo ambacho kinawanyima wafungwa na mahabusu fursa ya kuonana na ndugu au mawakili wao kutokana na umbali uliopo ambapo kutokana na juhudi za Mkuu wa Wilaya hiyo tayari Bweni moja la Wafungwa lenye uwezo wa kuhifadhi waha;lifu 150 limekamilika pamoja na Ofisi ya Utawala na ujenzi wa Ukuta wa gereza unaendelea katika Kambi hiyo ya Mkwajuni.