Na
ASP Deodatus Kazinja, Dodoma.
Wataalam
wa afya wa vituo vya magereza nchini
wameaswa kufanya kazi kwa weledi na juhudi kubwa ili kutimiza malengo
yanayotarajiwa na jeshi la magereza na taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike wakati
wa ufunguzi wa mkutano wa siku moja wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya Jeshi
la Magereza uliofanyika katika Ukumbi wa Morena Hoteli leo jijini Dodoma.
Aidha,
CGP Kasike amemuagiza Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza kufuatilia kwa ukaribu
utendaji wa kituo kimoja kimoja na kuhakikisha wataalam waliopo jeshini
wanafanya kazi zao kwa uweledi ikiwa ndiyo matarajio ya jeshi.
Wakati
huo huo CGP amewatolea wito wataalam hao wa afya magerezani kuhakikisha
wanatekeleza muongozo wa serikali unaoagiza kuwaanzishia dawa watu wote
wanaogundulika kuwa na maambukizi ya VVU na kuhakikisha wanakuwa na ufuasi
mzuri wa dawa.
Waganga
wakuu wa vituo vya afya katika Jeshi la magereza wapo katika mkutano huo unaofadhiliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya
JSI AIDS Free ukiwa na lengo la kufanya
tathmini ya mwenendo wa Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo
vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18.
Asasi
ya JSI AIDS Free chini ya serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Wizara ya
Mambo ya Ndani na Wziara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
kwa miaka minne sasa imekuwa ikishirikia na Jeshi la Magereza katika kuboresha Huduma
za Afya hasa mapambano ya Ukimwi.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP)
Phaustine Kasike akisalimiana na baadhi ya wajumbe na viongozi wa Asasi ya
kiraia ya JSI AIDS Free mara alipowasili leo Desemba 4, 2018 katika viwanja vya Morena Hotel jijini Dodoma
kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha siku moja cha kutathmini ya mwenendo wa Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi
katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akitoa hotuba katika
mkutano wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza yote nchini
kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free kwa ajili ya kutathmini ya mwenendo wa Mradi
Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza
kwa mwaka 2017/18 leo Desemba 4, 2018 Morena Hoteli jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma
SACP Omary Salum, Mtendaji Mkuu wa AIDS Free Tanzania Dkt. Deogratias Kakiziba.
Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza INSP Adili
Kachima na wapili kulia ni SSP Dkt.
Richard Mwakina kutoka kituo cha afya chama magereza Ukonga, Dar es salaam.
Washiriki
wa kikao wakifuatilia hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike
(hayupo pichani) katika kikao cha waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza
nchini kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free kwa ajili ya ufuatiliaji wa mwenendo wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi
katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18 kilichofanyika
leo tarehe 04 Desemba, 2018 jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Gereza Kuu
Butimba Mwanza ASP. Dkt. Alex Lukuba
akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi (CGP Kasike) ikiwa ni utambuzi wa kufanya
vizuri kwa kituo anachokisimamia katika kusimamia masuala yahusuyo Ukimwi
katika kituo chake.
Kamishna
Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine
Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa
vituo vya afya vya magereza kote nchini na watendaji wakuu wa Asasi ya isiyo ya
kiserikali ya JSI AIDS Free ambayo ndiyo wafadhili wa Mradi Uimarishaji wa
Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya Magereza na polisi nchini. (Picha zote
na Jeshi la Magereza)