Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Phaustine Kasike(kulia) akimvalisha cheo Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Lipina Lyimo
kuwa Kamishina Msaidizi wa Magereza
katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya
Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Phaustine Kasike(kulia) akimvalisha cheo Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Merkiory Komba
kuwa Mrakibu wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo
cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2019.
Mrakibu wa Magereza, Merkiory Komba ni Msaidizi wa Mkuu wa Jeshi hilo.
Baadhi ya Maafisa waliopandishwa
vyeo katika ngazi mbalimbali wakiwa timamu kabla ya Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini, Phaustine Kasike kuwasili kwa zoezi la uvishaji vyeo , jana
Agosti 6, 2019 kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga
jijini Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Phaustine Kasike(kulia) akikagua Gwaride maalum kabla ya zoezi la uvishaji vyeo kwa Maafisa wa
Mkoa wa Dr es Salaam na Mkoa wa Pwani
waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni.
Gwaride maalum likipita kwa
mwendo wa pole mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani)
kwenye hafla ya uvishaji vyeo kwa maafisa wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa
Pwani jana Agosti 6, 2019.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Maofisa wa ngazi mbalimbali wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo
(waliosimama)baada ya hafla uvishaji vyeo iliyofanyika katika viwanja vya Chuo
cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6,
2018(Picha zote na Jeshi la Magereza).