Waziri
Mkuu wa Tanzania Mh. Khasim Majaliwa akihutubia katika ufunguzi wa wiki ya
Elimu ya Sheria ambapo kitaifa yanaendelea kufanyika Jijini Dodoma, kaulimbiu ni utoaji haki ni
jukumu la mahakama na wadau.
Waziri
Mkuu wa Tanzania Mh. Khasim Majaliwa akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh.Profesa Ibrahim Juma Jaji Mkuu wa Tanzania
, Mh. Tulia Akson Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.B. Mahenge Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika
matembezi ya ufunguzi wa wiki ya Sheria yaliofanyika
asubuhi ya tarehe 02 Feb, 2019 Jijini Dodoma ambapo yalianzia katika viwanja
vya Mahakama Kuu na kuishia katika viwanja vya Nyerere Squire.
Maafisa wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu ya Magereza
, Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma na Gereza Kuu Isanga wakiwa katika matembezi ya wiki ya elimu ya
sheria jijini Dodoma kutoka kushoto ni
Kamishna wa Magereza anayesimamia Fedha
na Mipango (CP) Gideon Nkana , Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Salum
Hussein, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Rajabu Nyange,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza(SACP) Mzee Ramadhan Nyamka, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi (SACP) Chacha Jackson Bina, Mkuu wa Gereza Kuu Isanga Kamishna Msaidizi wa
Magereza(ACP) Keneth Mwambije.
Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini Mrakibu wa Magereza (SP)
Amina Kavirondo akimpa ufafanuzi Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Khasim Majaliwa kuhusu masuala ya
haki na ulinzi wa watoto walioko Magerezani kutokana na Mama zao kukinzana na
sharia.
Baadhi ya Maafisa na askari wa jeshi la Magereza
wakishiriki katika matembezi ya maadhimisho ya wiki ya sheria Dodoma.( picha na
Cpl Mfaume Ally- Jeshi la Magereza)