Banner

Banner

Tuesday, February 16, 2016

Madereva wa magari ya jeshi la magereza nchini waaswa kuzingatia sheria za usalama barabarani, mkoani Morogoro

Kamishna Jenerali John Casmir Minja akipokea Salaam ya Utii kutoka kwa Gadi Maalam iliyoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza, Wahitimu wa Mafunzo ya Udereva(hawapo pichani) katika Chuo cha Udereva Kingolwira Mkoani Morogoro. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo hicho 16 Februari, 2016.
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum iliyoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Udereva katika Chuo cha Uderevau na Ufundi Kingolwira, Mkoani Morogoro.
Wahitimu wa Mafunzo hayo wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika mwendo wa kasi kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akipokea taarifa fupi Ofsini kwa Mkuu wa Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Osmond Nduguru(hayupo pichani).
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akimtunuku cheti Askari Mhitimu wa Mafunzo ya Udereva kwa niaba ya Wahitimu wote wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Mkoani Morogoro wakifanya Mahojiano Maalum na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Mgeni rasmi, Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Mafunzo ya Udereva katika Chuo cha Udereva na Ufundi, Kingolwira Mkoani Morogoro.

Na Lucas Mboje; Morogoro

MADEREVA wote wa magari ya Jeshi la Magereza nchini wametakiwa kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani wakati wote wanapoendesha magari ili kujiepusha na ajali zisizo za lazima.

Rai hiyo imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja wakati akizungumza kwenye hafla ya kufunga Mafunzo ya Udereva Kozi ya Msasa kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa yote Tanzania Bara yaliyofanyika katika Chuo cha Udereva na Ufundi, Kingolwira Mkoani Morogoro.

Jenerali Minja amewaagiza Wahitimu wa Mafunzo hayo kuhakikisha kuwa wanawajibika pia kuyatunza magari watakayokabidhiwa kuyaendesha ili yaweze kudumu kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa.

"Nawataka mjiepushe na uzembe wakati mnapoendesha magari ya Jeshi letu ikiwa ni pamoja na kutokujihusisha na ulevi na kuendesha magari hayo kwa mwendo kasi bila kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani". Alisema Jenerali Minja.

Aidha Jenerali Minja amezungumzia upungufu mkubwa wa magari katika Jeshi hilo ambapo katika kushughulikia changamoto hiyo Jeshi la Magereza kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa limesaini Mkataba na Kampuni za Ashok Layland na Jeep na magari mia tisa na tano(905) yanategemewa kupokelewa mapema mwanzoni mwa mwezi Mei Mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Osmond Ndunguru kupitia risala yake kwa Mgeni rasmi amesema kuwa Wahitimu hao wamejifunza Mafunzo yote yaliyopo kwenye Mtaala wa Mafunzo ya Udereva kwa nadharia na vitendo ikiwemo mbinu mbalimbali katika fani ya Udereva wa Magari ambapo jumla ya Wanafunzi 125 wamehitimu Mafunzo hayo miongoni mwao Wanaume ni 133 na wa kike ni 2.

Aidha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Nduguru alieleza changamoto mbalimbali ambazo Chuo hicho kinakabiliana nazo ikiwemo upungufu wa magari ya kujifunzia pamoja na uchakavu wa miundombinu ya majengo hali inayoathili utoaji taaluma ya mafunzo hayo.

Chuo cha Udereva na Ufundi cha Kingolwira, kilichopo Mkoani Morogoro kinamilikiwa na Jeshi la Magereza ambacho hutoa Mafunzo ya Udereva kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza ambao huendesha magari ya Jeshi hilo na katika Taasisi mbalimbali za Umma hapa nchini.

Friday, February 5, 2016

Ujumbe kutoka chuo cha ulinzi wa taifa watembelea makao makuu ya jeshi la magereza jijini Dar

Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016(kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisalimiana na Mkufunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa ambaye ni raia kutoka China(katikati) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiongea na Ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani). Ujumbe huo wa Washiriki wa Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza  katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza hapa nchini.
Wakunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati yao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Washiriki wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa walipotembelea Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kwa ziara yao ya Mafunzo(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Mwandamizi wa Magereza, Augustine Mboje.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kutoka chuo cha Ulinzi wa Taifa wakImwangalia mmoja wa wafungwa ambaye amepatiwa ujuzi gerezani wa kukata vitambaa vya nguo tayari kwa kushona nguo za wafungwa wliopo magerezani kama anavyoonekana katika picha katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahiriki wa Mafunzo(waliosimama mstari wa nyuma) walipotembelea Jeshi la Magereza kujifunza uendeshaji wa Jeshi hilo(wa nne kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)

Thursday, February 4, 2016

Kamishna jenerali wa magereza John Casmir Minja ashiriki maadhimisho ya siku ya sheria nchini, jijini Dar

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Othman Chande akiwaongoza Maandamano ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuelekea katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo Februari 04, 2016, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli(hayupo pichani). kulia ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Poilisi, Abdulrahmani Kaniki(kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa hotuba yake fupi katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo Februari 04, 2016, Jijini Dar es Salaam.
Wageni Waalikwa na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Sheria wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Othman Chande akitoa hotuba yake fupi katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo Februari 04, 2016, Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama/Wawakilishi wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliohudhuria Maadhimisho hayo ya Siku ya Sheria nchini(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Kidini na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama(waliosimama msatari wa nyuma)katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo Februari 04, 2016, Jijini Dar es Salaam(wa nne kushoto) ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Othman Chande(wa tatu kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Harrison Mwakyembe(wa nne kulia) ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. TULIA Mwansasu.
Bendi ya Jeshi la Poilisi ikiongoza Maandamano ya Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo Februari 04, 2016, Jijini Dar es Salaam

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza). 

Monday, February 1, 2016

Mkurugenzi mkuu wa tume ya ushindani akabidhi vifaa vya muziki kwa jeshi la magereza jijini, Dar

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akitoa maelezo mafupi kwenye hafla ya  makabidhiano ya vifaa vya muziki kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo ilifanyikia Bwalo Kuu la Maafisa  Magereza, Ukonga  Jijini Dar es salaam, Januari 29, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja gitaa la muziki ikiwa ni moja wapo ya vifaa vya muziki vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza
Kamishna Jenerali wa Magereza akijaribisha kupiga gitaa la muziki baada ya kukabidhiwa vifaa vya muziki katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(wa kwanza kulia).
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo kwenye hafla ya  makabidhiano ya vifaa vya muziki ambavyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi la Magereza.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani,  Dkt. Fredrick Ringo(hayupo pichani). 
Baadhi ya vifaa vya muziki venye vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza kama vinavyoonekana katika picha. Vifaa hivyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi hilo

(Picha na Kitengo cha Habari, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).