Banner

Banner

Monday, September 23, 2019

KAMISHNA JENERALI PHAUSTINE KASIKE ARIDHISHWA NA UJENZI WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU, GEREZA KUU ISANGA TAREHE 21 SEPT 2019

 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mkoani Dodoma alipowasili kwenye ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga, Septemba 21, 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(mwenye miwani) akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga,  Septemba 21, 2019. Kulia kwake ni Mkuu wa Magereza mkoani Dodoma, ACP. Keneth Mwambije.

Muonekano wa nyumba takribani 20 ambazo tayari zimejengwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga zikiwa katika hatua mbalimbali ya ujenzi.

Tofali za kuchoma zikiwa tayari katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga.

Wafungwa wa Gereza Kuu Isanga wakiendelea na kazi ya ujuenzi katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika Gereza Kuu Isanga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa program ya Urekebishaji magerezani.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(mwenye miwani) akiangalia mbao zinazotumika katika hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi ya Maafisa na askari katika                               Gereza Kuu Isanga, alipotembelea eneo hilo la ujenzi, Septemba 21, 2019.                                   (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Monday, September 2, 2019

MAKAMISHNA WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA WALIOSTAAFU UTUMISHI WAO KWA MUJIBU WA SHERIA, WAAGWA JIJINI DAR TAREHE 31/09/2019

Kamishna Mstaafu wa Magereza, Gedion Nkana(kushoto) na Kamishna Mstaafu wa Magereza, Augustine Mboje(kulia) wakiwa kwenye gari maalum wakipita katikati ya Gwaride likiwa katika umbo la OMEGA ikiwa ni ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wao Jeshini. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam Agosti 30, 2019.

Makamishna Wastaafu wa Magereza wakipita katika gari maalum wakiwapungia mikono Maafisa na askari pamoja na Wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Agosti 30, 2019
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kushoto) akiwa na Maafisa Waandamizi kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini wakiwapungia mikono  Makamishna Wastaafu wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Agosti 30, 2019.

Kamishna Mstaafu wa Magereza, Gedion Nkana akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo leo Agosti 30, 2019.

Gwaride maalum lililoundwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza likipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Makamishna Wastaafu wa Jeshi hilo ambao wamestaafu utumishi wao kwa mujibu wa Sheria.
Kamishna Mstaafu wa Magereza, Gedion Nkana(kushoto) na Kamishna Mstaafu wa Magereza, Augustine Mboje(kulia) wakiwa katika jukwaa kuu wakipokea salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride maalum la kuwaaga leo Agosti 30, 2019 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, John Casmir Minja mara baada ya gwaride maalum la kuwaaga Makamishna wastaafu wa Jeshi hilo ambao wamestaafu utumishi wao Jeshini kwa mujibu wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Jenerali Wastaafu wa Jeshi la Magereza(walioketi) pamoja na Makamishna Waliopo wa Jeshi Magereza, Makamishna Wastaafu wa Magereza na Maafisa Waandamizi wastaafu wa Jeshi la Magereza(waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya ya Gwaride rasmi la kuwaaga Makamishna Wastaafu wa Jeshi hilo leo Agosti 30, 2019(Picha  zote na Jeshi la Magereza).