Banner

Banner

Tuesday, October 7, 2014

President of the Asian Injury Prevention Foundation (AIP)/ Global Helmet Vaccine Initiative holds official talks with the permanent secretary in the Prime Minister’s office in Dar es Salaam

 The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(centred) and the President of Assian Injury Prevention Foundation, Creig Craft(third right) during the Official talks held in Prime Minister's Office this afternoon concerns about the support of government to the Helmet factory project expected to take off at Ukonga Central Prison in Dar es Salaam.
 President of Assian Injury Prevention Foundation, Creig Craft(third right) in conversation with his host The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(not in picture). The first right is the Agro Economist, Superitendent of Prisons, Uswege Mwakahesya(centered) is the Chief Executive Officer of the Helmet Vaccine Inniciative Tanzania, Mr. Alpherio Nchimbi.
 The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka held talks concerns the support of government to the Helmet factory project expected to take off at Ukonga Central Prison in Dar es Salaam.
 The Chief Executive Officer of Tanzania Prisons Cooperation Sole, Senior Assistant Commissioner of Prisons, John Masunga(right) listens a comment from the The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(left) is Mr. Asanterabi Sang'enoi, Assistant Director in the Prime Minister's Office.
 The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(right) shares a light moment with the  Chief Executive Officer of Tanzania Prisons Cooperation Sole, Senior Assistant Commissioner of Prisons, John Masunga(left)after an Official talks about the support of government to the Helmet factory project expected to take off at Ukonga Central Prison in Dar es Salaam.
 The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(centred) in a group photo with the President of Assian Injury Prevention Foundation, Creig Craft(third right) during the Official talks held in Prime Minister's Office in Dar es Salaam this afternoon. Others are Senior Prisons Officers' who accompanied the President.
The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(right) accompany the President of Assian Injury Prevention Foundation, Creig Craft(left) after the Official talks held in Prime Minister's Office this afternoon concerns about the support of government to the Helmet factory project expected to take off at Ukonga Central Prison in Dar es Salaam.

Thursday, October 2, 2014

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania afunga rasmi mafunzo ya ulinzi wa amani kwa maafisa magereza toka nchi za SADC, mkoani Kilimanjaro


 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati meza Kuu) akisikiliza maelezo mafupi toka kwa Mratibu wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Kanali Sambulo Ndrovu(hayupo pichani) kabla ya kufunga rasmi Mafunzo hayo leo Oktoba 02, 2014. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa pili kulia) ni Mratibu Msaidizi wa Mafunzo hayo Kamishna Msaidizi wa Magereza toka Nchini Zimbabwe, Didmas Chimvura(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani ambayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo jumla ya Maafisa Magereza 27 toka Nchi za SADC ikiwemo Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Mauritius, Swaziland na Zimbabwe wameshiriki kikamilifu Mafunzo hayo.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Mkaguzi wa Magereza Nchini Tanzania, Pendo Kazumba. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili na yameendeshwa na Kituo cha Mafunzo cha SADC kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania(kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC Bregedia Jenerali Christopher Chellah.
 Wakufunzi wa Mafunzo hayo wakisikiliza hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC. Jumla ya Wahitimu 27 toka Nchi za SADC wameshiriki Mafunzo hayo kikamilifu katika Chuo cha Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa kwanza kulia) ni Mratibu wa Mafunzo hayo, Kanali Sambulo Ndlovu toka Zimbabwe(wa pili kulia) ni Mkufunzi toka Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Charles Novart(wa tatu kushoto) ni Mkufunzi toka Tanzania, Ahmad Mwidadi(wa pili kulia) ni Mkufunzi toka Zambia, Mrakibu wa Polisi Nchini Zambia, Edward Njovu.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari toka Vyombo vya TBC1 na ITV Mkoani Kilimanjaro mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC leo Oktoba 2, 2014 Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa sita kulia) na Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Magereza Wanawake toka Nchi za SADC ambao wameshiriki kikamilifu Mafunzo ya wiki mbili ya Ulinzi wa Amani katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(kushoto) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(kulia) mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC(katikati) ni Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo hayo toka Nchini Tanzania, Mkaguzi wa Magereza, Pendo Kazumba.

Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Magereza toka Nchi za SADC(waliosimama) walioshiriki Mafunzo ya Ulinzi wa Amani ambayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro. Mafunzo hayo yamefungwa leo na Kamishna Jenerali wa Magereza ambapo jumla ya Maafisa Magereza 27 toka Nchi za SADC ikiwemo Tanzania, Mauritius, Afrika Kusini, Swaziland, Botswana, Namibian na Zimbabwe wamehitimu Mafunzo hayo Maalum ya Ulinzi wa Amani(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Monday, September 29, 2014

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Tanzania ashiriki maadhimisho ya Magereza Day nchini Zambia

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa tatu kulia) akisalimiana na Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini Zambia, Mhe. Nickson Chilangwa(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela. Maadhimisho hayo yamefanyika Septemba 26, 2014 katika Viwanja Vya Chuo Cha Maafisa Magereza Mjini Kabwe, Zambia.
Baadhi ya Maafisa na Askari Magereza na wageni wengine Waalikwa wakifutilia matukio mbalimbali yaliyofanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa na Askari Kabwe, Zambia.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja akiongozana na Wakuu Wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Zambia kuelekea kwenye Jukwaa Kuu kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela.
 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa Nne kulia Jukwaa Kuu) akiwa na Wakuu Wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Zambia wakipokea Salaamu ya heshima kutoka kwa Maafisa na Askari Magereza Nchini Zambia(hawapo pichani)wakati Gwaride hilo likipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa pole na haraka katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini Zambia, Kamishna Percy Chato
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Magereza Nchini Zambia, Kamishna Percy Chato wakiaangalia kazi za aina mbalimbali zinazofanywa na Wafungwa wa Zambia katika Mabanda mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia.
 Gadi Maalum ya Maafisa na Askari Magereza wa Nchini Zambia wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo haraka katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia yaliyofanyika Septemba 26, 2014.
 Kwaya ya Wafungwa wa Nchini Zambia wakitoa Burudani ya nyimbo za Injili wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia yaliyofanyika Septemba 26, 2014.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Zambia, Mhe. Nickson Chilangwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Urekebishaji/Magereza Afrika(walioketi). Wa Nne kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa tano kulia) ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini Zambia, Percy Chato(wa tatu kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela(Picha zote na Kitengo cha Habari Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).