Banner

Banner

Thursday, November 14, 2019

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AKAGUA UJENZI WA MAKAZI YA MAOFISA MAGEREZA UKONGA, APONGEZA HATUA KUBWA ILIYOFIKIWA TAREHE 13 NOVEMBA,2019

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Maafisa wa SUMAJKT pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza alipowasili katika eneo la ujenzi Gereza Kuu Ukonga Novemba 13, 2019 katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua ujenzi unaoendelea wa makazi ya Maafisa na askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Ofisa wa SUMAJKT, Meja Ashrafu Hassan akitoa taarifa fupi kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike alipotembelea  Novemba 13, 2019 kwa lengo la kukagua ujenzi huo.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua ujenzi wa majengo mbalimbali ya makazi ya Maafisa na Askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga. Kulia kwake ni Ofisa wa SUMAJKT, Meja Ashrafu Hassan akimuonesha baadhi ya maeneo ambayo bado yanafanyia maboresho ya miundombinu.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua miundombinu ya mitaro ya kupitishia maji ya mvua katika ujenzi wa majengo mbalimbali za makazi ya Maafisa na Askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga.

Moja ya majengo ya ghorofa yaliyojengwa kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Magereza katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, jijini Dar es Salaam yakiwa tayari yamekamilika kama inavyoonekana katika picha (Picha na Jeshi la Magereza).

Thursday, November 7, 2019

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA MRADI WA KOKOTO GEREZA MSALATO, MKOANI DODOMA





Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiongea na Wafungwa wa Gereza Msalato(hawapo pichani) wanaofanya kazi za uzalishaji kokoto katika mradi huo wa Gereza hilo. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua moja ya eneo la kulipulia mawe ya kokoto katika eneo la Gereza Msalato leo alipofanya ziara ya kikazi.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiangalia mtambo wa uzalishaji katika mradi wa uzalishaji kokoto wa Gereza Msalato, Dodoma leo alipofanya ziara ya kikazi.  Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA)  limewekeza  mradi  huo wa kokoto katika eneo la Gereza Msalato, Mkoani Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(aliyevaa miwani) akiangalia kokoto  zinazozalishwa katika mradi huo wa Gereza Msalato leo alipofanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije na Kulia ni Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Huruma Mwalyaje.

Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Huruma Mwalyaje(katikati) akimwelezea jambo Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) kabla ya kutembelea eneo la mradi wa uzalishaji kokoto. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Wednesday, November 6, 2019

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, PHAUSTINE KASIKE, LEO JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike  akisaini kitabu cha Wageni alipomtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai(hayupo pichani), leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike  alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma kwa mazungumzo maalum.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Kamishna Jenerali wa  Magereza nchini, Phaustine Kasike  mara baada ya mazungumzo alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Job Ndugai (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni, Jijini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Keneth Mwambije               (Picha zote na Jeshi la Magereza).