Banner

Banner

Wednesday, November 5, 2014

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi afungua mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza katika Hoteli ya Livingstone-Bagamoyo

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil akitoa hotuba fupi ya Ufunguzi wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Wadau wakifuatilia kwa Makini Majadiliano ya maoni kuhusu  maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi katika ufunguzi wa  Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Wadau wakifuatilia kwa makini maelezo ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika Ufunguzi wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Mshauri Mwelekezi, Dkt. Haji Semboja toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyeshiriki kikamilifu kuandaa Rasmu ya Sera ya Taifa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Wataalam wa Jeshi la Magereza akiwasilisha rasimu hiyo leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo kabla ya kuanza majadiliano.
Inspeketa Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema(kulia) akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari kutoka Vyombo vya ITV na Channel Ten leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(wa pili kulia) akiteta jambo na Inspeketa Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema(kulia) baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza(kulia) akimuongoza  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(kushoto) alipowasili kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza.
Inspeketa Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema(wa kwanza kushoto) akifuatilia kwa Makini Majadiliano ya maoni kuhusu  maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo. Wengine kulia ni Viongozi Wastafu wa Jeshio la Magereza.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawaki(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki Wadau wa Mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Sera ya Taifa ya Jeshi la Magereza ulioanza leo Novemba 04, 2014 katika Hoteli ya Livingstone - Bagamoyo.

Wednesday, October 22, 2014

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza akabidhi zawadi ya basi dogo Bwawani Sekondari katika mahafali ya kumi na moja ya kidato cha nne yaliyofanyika mkoani Pwani

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akikabidhi funguo za Basi dogo kwa Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga(kushoto). Basi hilo litatumiwa na Wanafunzi katika ziara mbambali za Mafunzo hivyo kuondoa kero kubwa ya Usafiri shuleni hapo.
Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani Sekondari, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga akijaribisha kuwasha gari jipya lililokabidhiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika Mahafali ya Kumi na moja ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari yaliyofanyika leo Oktoba 22, 2014.
Muonekano wa Basi dogo lenye Na. MT. 0341 lililokabidhiwa leo Oktoba 22, 2014 na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani. Basi hilo litatumiwa na Wanafunzi wa Bwawani Sekondari katika ziara mbalimbali za Mafunzo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(aliyevaa skafu) akiwa meza Kuu amesimama na Viongozi mbalimbali Waalikwa wakati Wahitimu Wakiimba Wimbo Maalum wa Shule katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari leo Oktoba 22, 2014(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunula (wa kwanza kulia) ni Kaimu Mkuu wa Shule ya Bwawani Sekondari, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa Mhitimu wa Kidato cha Nne katika Mahafali ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari leo Oktoba 22, 2014. Jumla ya Wahitimu 95 wametunukiwa cheti cha kuhitimu Elimu ya Kidato cha Nne katika Shule hiyo inayomilikiwa na Jeshi Magereza, Mkoani Pwani.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Casmir Minja akitoa hotuba yake fupi katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne Bwawani Sekondari yaliyofanyika leo Oktoba 22, 2014 Mkoani Pwani.
Sehemu ya Wahitimu katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne, Bwawani Sekondari wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi, Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani).
Kikundi cha Wasanii kinachoundwa na Wanafunzi wa Bwawani Sekondari kikijiandaa kutumbuiza mbele ya Mgeni rasmi katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato cha Nne Shule ya Bwawani Sekondari, Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014, Mkoani Pwani.
Mama mzazi wa Mhitimu wa Kidato cha Nne kutoka familia ya Kifugaji ya Kimasai akimbusu mkono Mtoto wake ambaye amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne katika Shule inayomilikiwa na Jeshi la Magereza, Bwawani Sekondari iliyopo Mkoani Pwani. Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa na Wahitimu wa Kidato cha Nne katika Mahafali ya Kumi na moja ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Bwawani inayomilikiwa na Jeshi la Magereza. Mahafali hayo yamefanyika leo Oktoba 22, 2014 katika Bwalo la Bwawani Sekondari, Mkoani Pwani

(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Monday, October 20, 2014

Kamishna Jenerali wa Magereza Minja awaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa afisa mnadhimu mkuu msaidizi wa Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisaini katika Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ambaye amefariki Jumapili tarehe 19 Oktoba, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
 
Mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ukiwa umebebwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya kuagwa rasmi leo Oktoba 20, 2014 nyumbani kwake, Ukonga Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa amesimama wakati mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ulipowasili tayari kwa kuuagwa rasmi nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2014(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Nicas Banzi(wa pili kushoto) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Jumanne Mangara(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa
 Mchungaji wa Kanisa la Moravian lililopo Ukonga, Banana Relini Hansi Mwakijoja akiwaongoza Waombolezaji kwa sala kabla ya kuuaga rasmi mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
 Baadhi ya Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa wamejipanga katika mstari tayari kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza leo Oktoba 20, 2014 Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu unatajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Tutuo Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora kwa Mazishi.
 Mke wa Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza akiwa na majonzi makubwa na waombolezaji kabla ya kuuaga rasmi mwili wa mume wake ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
 Sehemu ya Waombolezaji waliojitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini wasifu wa Marehemu kabla ya kuuaga rasmi leo Oktoba 20, 2014 Ukonga, Dar es Salaam.
 Bendi ya Jeshi la Magereza ikitumbuiza katika hafla fupi ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).