Kamishna Jenerali wa Magereza Jonn Minja (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (GEPF) Bw. Daud Msangi (kulia) Alhamis 29, 2014
Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Bw. Daud Msangi Mkurugenzi Mkuu wa GEPF (kulia) wakisaini Mkataba wa Uwekezaji baina ya Taasisi hizo mbili leo Alhamis 29 Mei, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Jijini Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Bw. Daud Msangi Mkurugenzi Mkuu wa GEPF (kulia) wakikabidhiana nyaraka za makubaliano ya uwekezaji baada ya kutiwa sahini.leo Alhamis 29 Mei, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Shirika la Magereza ( Prisons Corporation Sole) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) John Masunga (kushoto) pamoja na Mwanasheria wa GEPF Anna Shayo (kulia) wakisaini nyaraka muhimu za makubaliano ya uwezekaji kati ya Magereza na GEPF).
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria hafla ya utiliwaji sahini wa Mkataba wa Uwekezaji kati ya Jeshi la Magereza na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa GEPF. Waliokaa ni Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw.Daud Msangi (kulia). Kutoka kushoto ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Kizito Jaka, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) John Masunga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Gideon Nkana, Festo Fute (GEPF), Anna Shayo (GEPF) na Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Issack Kangura.
Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja wa Magereza
Na Deodatus Kazinja-PHQ
Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la uzalishaji mali (Prisons Corporation Sole) limetiliana Mkataba wa uwekezaji na Mfuko wa Jamii wa GEPF ambapo majengo ya vitega uchumi yatajengwa katika maeneo ya Kihonda Mkoani Morogoro na Karanga Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Tukio hilo la utiwaji sahini mkataba huo limefanyika leo Alhamis 29, 2014 katika ukumbi wa mikutano ulioko Makao Makuu ya Jeshi la
Magereza Jijini Dar es salaam. Akiongea katika hafla hiyo Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja amesama ni kiu yake kuona mradi huo unaanza kutekelezwa ifikapo Julai Mosi, 2014. Naye Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw. Daud Msangi amesema ukiwepo ushirikiano wa kutosha miradi hii itaweza kukamilika mapema iwezekanavyo kwa faidi ya pande zote mbili.