Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja
akisisitiza jambo katika mazungumzo na Ujumbe Maalum kutoka Kampuni ya
Equator Automech inayojishughulisha na uunganishaji Magari na Matrekta
hapa Nchini. Kampuni hiyo ipo katika mazungumzo ya Awali ya kuingia Ubia
na Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza katika miradi
mbalimbali ya Uzalishaji ikiwemo ya Kilimo. Ujumbe huo umefanya
mazungumzo hayo leo Agosti 13, 2014 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Equator Automech, Robert
Ndege(wa kwanza kushoto) akielezea namna Kampuni yake itakavyoshrikiana
na Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza katika miradi
mbalimbali ya Uzalishaji ikiwemo ya Kilimo(katikati) ni Mkurugenzi
Mshauri wa Kampuni hiyo, Ahmed Bakari akifuatilia mazungumzo hayo.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo ya
namna Kampuni ya Equator Automech itakavyoshrikiana na Jeshi la
Magereza kupitia Shirika lake la Magereza katika miradi yake ya Kilimo.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Agosti 13, 2014 Jijini Dar es Salaam(wa
kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza,
Gaston Sanga(katikati) ni Mkuu wa Kitengo cha Kilimo na Mifugo, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro(wa kwanza kushoto) ni
Mthibiti wa Fedha wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Gideon Nkana(wa pili kushoto) ni Mwanasheria wa Jeshi la
Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Issack Kangura(Picha zote na
Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).