Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja
akiongoza Kikao cha Mazungumzo ya Awali na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, Bw. William Erio(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji
katika maeneo ya Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio
akifanya mazungumzo ya Awali na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo
ya Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara Agosti 11, 2014
Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia
mazungumzo ya Awali na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw William Erio(hayupo
pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza Mikoa ya
Dar es Salaam na Mtwara(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) ni Kamishna wa Fedha
na Utawala, Gaston Sanga(Kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la
Magereza, Solomon Urio akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir
Minja(kushoto) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Bw. William Erio eneo linalofaa Uwekezaji wa Hoteli kubwa ya Kimataifa
lililopo Ukonga, Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa PPF amefanya
mazungumzo ya Awali na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza kuhusu
Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza Agosti 11, 2014 Jijini Dar
es Salaam
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini John Casmir Minja
akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William
Erio(kulia) mara tu baada ya kufanya mazungumzo ya Awali kuhusu
Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza katika Mikoa ya Dar es
Salaam na Mtwara. Mkurugenzi Mkuu wa PPF amefanya mazungumzo hayo
Agosti 11, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es
Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).