Banner

Banner

Monday, September 29, 2014

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Tanzania ashiriki maadhimisho ya Magereza Day nchini Zambia

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa tatu kulia) akisalimiana na Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini Zambia, Mhe. Nickson Chilangwa(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela. Maadhimisho hayo yamefanyika Septemba 26, 2014 katika Viwanja Vya Chuo Cha Maafisa Magereza Mjini Kabwe, Zambia.
Baadhi ya Maafisa na Askari Magereza na wageni wengine Waalikwa wakifutilia matukio mbalimbali yaliyofanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa na Askari Kabwe, Zambia.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja akiongozana na Wakuu Wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Zambia kuelekea kwenye Jukwaa Kuu kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela.
 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa Nne kulia Jukwaa Kuu) akiwa na Wakuu Wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Zambia wakipokea Salaamu ya heshima kutoka kwa Maafisa na Askari Magereza Nchini Zambia(hawapo pichani)wakati Gwaride hilo likipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa pole na haraka katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini Zambia, Kamishna Percy Chato
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Magereza Nchini Zambia, Kamishna Percy Chato wakiaangalia kazi za aina mbalimbali zinazofanywa na Wafungwa wa Zambia katika Mabanda mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia.
 Gadi Maalum ya Maafisa na Askari Magereza wa Nchini Zambia wakipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo haraka katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia yaliyofanyika Septemba 26, 2014.
 Kwaya ya Wafungwa wa Nchini Zambia wakitoa Burudani ya nyimbo za Injili wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia yaliyofanyika Septemba 26, 2014.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Zambia, Mhe. Nickson Chilangwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Urekebishaji/Magereza Afrika(walioketi). Wa Nne kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa tano kulia) ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini Zambia, Percy Chato(wa tatu kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela(Picha zote na Kitengo cha Habari Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).


Saturday, September 20, 2014

Taarifa kwa vyombo vya Habari

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikiripotiwa na baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii kuhusiana na kunyanyaswa, kutendewa vitendo visivyo vya kiungwana na kuteswa gerezani kwa Watuhumiwa wa Makosa ya Ugaidi kinyume na taratibu za Uendeshaji wa Magereza.

Kufuatia tuhuma hizo, Jeshi la Magereza Tanzania Bara limefanya uchunguzi kwa kufanya mazungumzo na Watuhumiwa wenyewe na wamekanusha tuhuma hizo dhidi ya Jeshi la Magereza. Ukweli ni kuwa taarifa hizo si za kweli na hatuelewi kusudio lao ni nini.

Jeshi la Magereza Tanzania Bara linatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kuhusiana na Utunzaji wa Wahalifu na haki zao kwa kuzingatia misingi ya Haki za Binadamu. Vitendo vya kunyanyasa au kudhalilisha Wafungwa vinakemewa vikali magerezani na si Sera ya Jeshi la Magereza au Serikali.

Napenda kuufahamisha umma kuwa Mahabusu hao wanaotuhumiwa kwa Makosa ya Ugaidi wapo salama, wana Afya nzuri na hawana tatizo lolote gerezani.


Imetolewa na;

John Casmir Minja,
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
20 Septemba, 2014.

Tangazo la Ajira Mpya

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI 
(Jeshi la Magereza) 



TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA

Jeshi la Magereza Tanzania Bara linatangaza nafasi za Mafunzo ya Awali ya Askari Magereza yatakayoendeshwa Chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Mbeya. Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

MASHARTI YA KUAJIRIWA:

1.    JINSI:   Mvulana au Msichana ambaye hajawahi kuoa au kuolewa na asiwe na mtoto

2.    URAIA:            Awe Raia wa Tanzania Bara

3.    UMRI:
(a)  Wahitimu wa Shahada:    Awe na umri wa kati ya miaka 18 na 28
(b)  Wasio na Shahada:    Awe na umri wa kati ya miaka 18 na 24

4.    UREFU:

(a)   Wavulana: Wawe na urefu usiopungua Sentimeta 170.2 au Futi  5 na inchi 7
(b)   Wasichana: Wawe na urefu usiopungua Sentimeta 167.64 au Futi 5 na inchi 4
  
5.    SIFA NYINGINEZO:
i)   Awe amehitimu Elimu yake kati ya Mwaka 2012 na 2014
ii)   Awe na Afya nzuri iliyothibitishwa na Daktari anayetambuliwa na Serikali
iii)  Awe hajawahi kushtakiwa wala kupatikana kwa kosa lolote la jinai
iv)  Awe na tabia na mwenendo mzuri
v)   Awe hajawahi kuajiriwa mahali popote Serikalini

7.    ELIMU:
(a)   Wenye Shahada katika Fani au Taaluma zifuatazo:
(i)    Shahada ya Sheria (Laws)
(ii)    Utekelezaji wa Sheria (Law Enforcement)
(iii)   Takwimu (Applied Statistics)
(iv)   Uchumi na Mipango (Economic Planning)
(v)    Mazingira (Environmental Science and Management or Geography and Environment Studies)
(vi)   Usanifu Majengo (Architecture)
(vii)   Ukadiriaji Majengo (Building Economics)
(viii)  Mipango na Usimamizi Miradi (Project Planning and Management)
(ix)    Uhandisi wa Umeme (Electrical Engineering)
(x)     Uhandisi wa Mitambo ya Kilimo (Agricultural Engineering)
(xi)    Tiba ya Mifugo (Veterinary Medicine)
(xii)   Misitu  (Forestry)
(xiii)   Uchumi Kilimo (Agronomy)
(xiv)   Bima (Insurance)
(xv)    Uhasibu na Usimamizi wa Vyama Ushirika (Cooperative Management and Accountancy)
(xvi)    (Project Planning and Management)
(xvii)   Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering)
(xviii)   Sayansi ya Kompyuta (Computer Science)
(xix)    Udaktari wa Binadamu (Doctor of Medicine)
(xx)    Ualimu wa Masomo ya Sayansi kama Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati
(xxi)    Ualimu wa Masomo ya Biashara na Kifaransa (Commercial Subjects, Economics and French)
(xxii)    Ukutubi (Library and Information Studies)
(xxiii)    Mahusiano (Public Relations)
(xxiv)    Biashara na Masoko (Commerce in Marketing)

(b)    WASIO NA SHAHADA
1.1: Wenye Stashahada (Diploma) toka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i)    Ukutubi (Library)
(ii)   Uchumi na Mipango (Economic Planning)
(iii)   Bima (Insurance)
(iv)   Uhasibu na Usimamizi wa Vyama Ushirika (Co-operative Management and Accountancy)
(v)    Mipango na Usimamizi Miradi (Project Planning and Management)
(vi)   Utabibu (Clinical Medicine)
(vii)   Uuguzi (Nursing)
(viii)  Maabara (Laboratory Technician)
(ix)    Mazoezi ya viungo (Physiotherapy)
(x)    Uandishi wa Habari (Journalism)
(xi)   Ufundi Magari (Automobile Technician)
(xii)  Ujenzi (Civil Engineering)
(ix)   Umwagiliaji (Irrigation)
(x)    Mitambo ya Kilimo (Agro-Mechanics)
(xi)   Umeme (Electrical Engineering)
(xii)   Usanifu Majengo (Architecture)
(xiii)  Ushauri Nasaha (Counseling and Guidance)
(xiv)  Uhandisi Mitambo (Mechanical Engineering)
(xv)   Sanaa na Muziki (Fine and Performing Arts)
(xvi)  Ualimu wa masomo ya Biashara, Uchumi na Kifaransa

1.2:    Wenye Astashahada/ Cheti cha Majaribio ya Ufundi katika Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i)    Uhandisi Maji (Water Engineering)
(ii)    Ujenzi (Masonry)
(iii)    Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics)
(iv)    Umeme wa Magari (Auto-Electrical Engineering)
(v)    Waunganishaji Nondo (Steel Fixing)
(vi)    Useremala (Carpentry and Joinery)
(vii)    Bomba (Plumbing and Pipe Fitting)
(viii)    Rangi (Spray and Painting)
(ix)    Ushonaji (Tailoring)
(x)    Utengenezaji Sabuni (Soap Making)
(xi)    Ufumaji (Embroidery)
(xii)    Kutengeneza viatu (Shoe-Making)
(xiii)    Maabara (Laboratory Technician)
(xiv)    Uhitasi (Secretarial Studies with Computer Knowledge)
(xv)    Muziki na Utamaduni (Performing Arts and Music)
(xvi)    Uuguzi na Ukunga (Nursing and Midwife)
(xvii)    Utabibu Usaidizi (Clinical Assistant)

ZINGATIO:
Waombaji wa nafasi hizi wahakikishe wanazingatia masharti yote yaliyotajwa hapo juu. Upungufu au udanganyifu wowote utakaojitokeza kwa kutotimiza masharti yaliyotajwa hapo juu utasababisha maombi kutopokelewa na ikigundulika baada ya ajira mhusika atasitishwa mafunzo, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani.

8.    NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:

Waombaji wote watume maombi yao moja kwa moja kwa:-

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA,
MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA,
S.L.P 9190,
DAR ES SALAAM.

a)    Barua zote za maombi ziambatane na nakala za vyeti vyote vya elimu, ujuzi, Cheti cha kuzaliwa mwombaji na picha ndogo ya hivi karibuni ya mwombaji (Passport size photograph). Vyeti halisi na halali vitatakiwa kuoneshwa wakati wa usaili. Hati za matokeo ya mitihani (Results Slip/ Statement) hazitakubaliwa isipokuwa kwa wahitimu ambao vyeti vyao halisi havijatolewa na Vyuo husika pekee.

b)    Watakaofanikiwa kuitwa kwenye usaili watajulishwa kupitia katika Tovuti ya Jeshi la Magereza (www.magereza.go.tz), Magazeti na katika Mbao za matangazo zilizopo kwenye Ofizi za Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza lililopo Ukonga Dar es salaam.

c)    Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Oktoba, 2014.


KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
19 SEPTEMBA, 2014

Monday, September 15, 2014

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi azindua rasmi tovuti ya Jeshi la Magereza leo Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza tayari kwa uzinduzi rasmi wa TOVUTI ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akisalimiana na Mhe. Waziri(wa pili kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.                                                     
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(aliyesimama) akitoa maelezo mafupi kabla ya uzinduzi rasmi wa TOVUTI ya Jeshi la Magereza leo Septemba 15, 2014 katika Viwanja vya Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa TOVUTI ya Jeshi la Magereza, leo Septemba 15, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa TOVUTI ya Jeshi la Magereza kama wanavyoonekana katika picha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akikata utepe kabla ya kuzindua rasmi TOVUTI ya Jeshi la Magereza inayopatikana kupitia annuani ya www.magereza.go.tz(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Muonekano wa Mwanzo wa TOVUTI ya Jeshi la Magereza inayopatikana kupitia annuani ya www.magereza.go.tz

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).