JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Jeshi la Magereza)
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA
Jeshi la Magereza Tanzania Bara linatangaza nafasi za Mafunzo ya Awali ya Askari Magereza yatakayoendeshwa Chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Mbeya. Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
MASHARTI YA KUAJIRIWA:
1. JINSI: Mvulana au Msichana ambaye hajawahi kuoa au kuolewa na asiwe na mtoto
2. URAIA: Awe Raia wa Tanzania Bara
3. UMRI:
(a) Wahitimu wa Shahada: Awe na umri wa kati ya miaka 18 na 28
(b) Wasio na Shahada: Awe na umri wa kati ya miaka 18 na 24
4. UREFU:
(a) Wavulana: Wawe na urefu usiopungua Sentimeta 170.2 au Futi 5 na inchi 7
(b) Wasichana: Wawe na urefu usiopungua Sentimeta 167.64 au Futi 5 na inchi 4
5. SIFA NYINGINEZO:
i) Awe amehitimu Elimu yake kati ya Mwaka 2012 na 2014
ii) Awe na Afya nzuri iliyothibitishwa na Daktari anayetambuliwa na Serikali
iii) Awe hajawahi kushtakiwa wala kupatikana kwa kosa lolote la jinai
iv) Awe na tabia na mwenendo mzuri
v) Awe hajawahi kuajiriwa mahali popote Serikalini
7. ELIMU:
(a) Wenye Shahada katika Fani au Taaluma zifuatazo:
(i) Shahada ya Sheria (Laws)
(ii) Utekelezaji wa Sheria (Law Enforcement)
(iii) Takwimu (Applied Statistics)
(iv) Uchumi na Mipango (Economic Planning)
(v) Mazingira (Environmental Science and Management or Geography and Environment Studies)
(vi) Usanifu Majengo (Architecture)
(vii) Ukadiriaji Majengo (Building Economics)
(viii) Mipango na Usimamizi Miradi (Project Planning and Management)
(ix) Uhandisi wa Umeme (Electrical Engineering)
(x) Uhandisi wa Mitambo ya Kilimo (Agricultural Engineering)
(xi) Tiba ya Mifugo (Veterinary Medicine)
(xii) Misitu (Forestry)
(xiii) Uchumi Kilimo (Agronomy)
(xiv) Bima (Insurance)
(xv) Uhasibu na Usimamizi wa Vyama Ushirika (Cooperative Management and Accountancy)
(xvi) (Project Planning and Management)
(xvii) Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering)
(xviii) Sayansi ya Kompyuta (Computer Science)
(xix) Udaktari wa Binadamu (Doctor of Medicine)
(xx) Ualimu wa Masomo ya Sayansi kama Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati
(xxi) Ualimu wa Masomo ya Biashara na Kifaransa (Commercial Subjects, Economics and French)
(xxii) Ukutubi (Library and Information Studies)
(xxiii) Mahusiano (Public Relations)
(xxiv) Biashara na Masoko (Commerce in Marketing)
(b) WASIO NA SHAHADA
1.1: Wenye Stashahada (Diploma) toka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i) Ukutubi (Library)
(ii) Uchumi na Mipango (Economic Planning)
(iii) Bima (Insurance)
(iv) Uhasibu na Usimamizi wa Vyama Ushirika (Co-operative Management and Accountancy)
(v) Mipango na Usimamizi Miradi (Project Planning and Management)
(vi) Utabibu (Clinical Medicine)
(vii) Uuguzi (Nursing)
(viii) Maabara (Laboratory Technician)
(ix) Mazoezi ya viungo (Physiotherapy)
(x) Uandishi wa Habari (Journalism)
(xi) Ufundi Magari (Automobile Technician)
(xii) Ujenzi (Civil Engineering)
(ix) Umwagiliaji (Irrigation)
(x) Mitambo ya Kilimo (Agro-Mechanics)
(xi) Umeme (Electrical Engineering)
(xii) Usanifu Majengo (Architecture)
(xiii) Ushauri Nasaha (Counseling and Guidance)
(xiv) Uhandisi Mitambo (Mechanical Engineering)
(xv) Sanaa na Muziki (Fine and Performing Arts)
(xvi) Ualimu wa masomo ya Biashara, Uchumi na Kifaransa
1.2: Wenye Astashahada/ Cheti cha Majaribio ya Ufundi katika Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i) Uhandisi Maji (Water Engineering)
(ii) Ujenzi (Masonry)
(iii) Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics)
(iv) Umeme wa Magari (Auto-Electrical Engineering)
(v) Waunganishaji Nondo (Steel Fixing)
(vi) Useremala (Carpentry and Joinery)
(vii) Bomba (Plumbing and Pipe Fitting)
(viii) Rangi (Spray and Painting)
(ix) Ushonaji (Tailoring)
(x) Utengenezaji Sabuni (Soap Making)
(xi) Ufumaji (Embroidery)
(xii) Kutengeneza viatu (Shoe-Making)
(xiii) Maabara (Laboratory Technician)
(xiv) Uhitasi (Secretarial Studies with Computer Knowledge)
(xv) Muziki na Utamaduni (Performing Arts and Music)
(xvi) Uuguzi na Ukunga (Nursing and Midwife)
(xvii) Utabibu Usaidizi (Clinical Assistant)
ZINGATIO:
Waombaji wa nafasi hizi wahakikishe wanazingatia masharti yote yaliyotajwa hapo juu. Upungufu au udanganyifu wowote utakaojitokeza kwa kutotimiza masharti yaliyotajwa hapo juu utasababisha maombi kutopokelewa na ikigundulika baada ya ajira mhusika atasitishwa mafunzo, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani.
8. NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wote watume maombi yao moja kwa moja kwa:-
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA,
MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA,
S.L.P 9190,
DAR ES SALAAM.
a) Barua zote za maombi ziambatane na nakala za vyeti vyote vya elimu, ujuzi, Cheti cha kuzaliwa mwombaji na picha ndogo ya hivi karibuni ya mwombaji (Passport size photograph). Vyeti halisi na halali vitatakiwa kuoneshwa wakati wa usaili. Hati za matokeo ya mitihani (Results Slip/ Statement) hazitakubaliwa isipokuwa kwa wahitimu ambao vyeti vyao halisi havijatolewa na Vyuo husika pekee.
b) Watakaofanikiwa kuitwa kwenye usaili watajulishwa kupitia katika Tovuti ya Jeshi la Magereza (www.magereza.go.tz), Magazeti na katika Mbao za matangazo zilizopo kwenye Ofizi za Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza lililopo Ukonga Dar es salaam.
c) Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Oktoba, 2014.
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
19 SEPTEMBA, 2014