Mkurugenzi wa Mradi wa "AIDS free", Bw. Samson Kironde(wa pili kushoto) akitoa maelezo mafupi namna mradi huo utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza na Polisi katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza leo februari 20, 2015(wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Operesheni na Fedha, Bw. Mike Hames(wa kwanza kushoto) ni Afisa Mwandamizi anayeshughulikia masuala ya UKIMWI kutoka USAID, Bw. Erick Mlang'ha.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisisitiza jambo katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Polisi na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa "AIDS - free" utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioshriki katika mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa "AIDS - free" unaotarajiwa kutekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gedion Nkana(wa kwanza kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja.
Maofisa Wasimamizi wa Sekta ya Afya kutoka Jeshi la Polisi wakifuatilia mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa "AIDS - free"(wa kwanza kushoto) ni Dkt. Nyanda Lushina(katikati) ni Mrakibu wa Polisi, Husein Yahya.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(meza kuu) akiongoza mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa "AIDS - free" utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza