Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Botswana, Silas Motlalekgosi
akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wa Mkoani
Kilimanjaro alipotembelea Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi
leo Juni 25, 2015 akiwa na Viongozi Wakuu wa Taasisi za Urekebishaji/
Magereza kutoka Nchi za Swaziland, Uganda, Kenya, Zambia.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Swaziland, Isaya Ntshangase
akisaini kitabu cha Wageni alipowasili katika Kiwanda cha Viatu cha
Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo Viongozi hao wa Magereza kutoka Nchi za
Afrika wapo ziara ya kikazi nchini Tanzania.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile akitoa
utambulisho kwa Ujumbe wa Viongozi wa Magereza kutoka Nchi za Afrika
ambao wapo Nchini kwa ziara ya kikazi. Viongozi hao wametembelea Kiwanda
cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi.
Wafungwa wa Gereza Kuu Karanga Moshi wakiwa wanashona viatu aina ya Buti
ambavyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
hapa nchini kama wanavyoonekana katika picha wakishona sehemu ya juu ya
viatu hivyo. Wafungwa hao wa Gereza Kuu Karanga wananufaika na Stadi ya
Ushonaji viatu katika Kiwanda hicho kwa kujipatia ujuzi wa Ushonaji.
Muonekano
wa viatu aina ya Buti vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha
Gereza Kuu Karanga Moshi, viatu hivyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikiwa tayari vimekwishatengenezwa kama
vinavyoonekana katika picha.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).