S/N | JINA | KAMBI YA JKT ATOKAYO |
1 | RAPHAEL STEPHANO MWAMBASHI | ITENDE |
2 | RASHID MUSTAPHA MRAMBA | ITENDE |
3 | HAMZA MOHAMED MAKAIKA | ITENDE |
4 | SULTAN ABDALLAH MASSANJA | ITENDE |
5 | SALIMA BAKARI MAVUKILO | ITENDE |
6 | SALEHE ABBAS SALEHE | ITENDE |
7 | MOHAMED ADAM LUKWELLE | ITENDE |
8 | ALLY IAN BUGOYA | ITENDE |
9 | SIMON DAUDI REGATA | ITENDE |
10 | RAYMOND RAPHAEL NAKEI | ITENDE |
11 | PROSPER MATHIAS ASENGA | ITENDE |
12 | NICHOLAUS GODWIN MWAMBEBULE | ITENDE/RUVU |
13 | RASHID ABDALLAH MZIRAY | MGAMBO |
14 | REAGAN OCTAVIAN NGOWI | RUVU |
15 | ANDREW VITUS JOPHN | RUVU |
16 | YONA JOTHAM MWANGOKA | RUVU |
17 | PASCHAL CLEMENCE MTENGA | BULOMBORA |
18 | ISACK RICHARD HOYANGA | BULOMBORA |
19 | REBECCA SALIM GUMBO | BULOMBORA |
20 | JACKLINE AGRICOLA LIHIRU | BULOMBORA |
21 | MASOKA KITWARA ELLY | BULOMBORA |
22 | KAMSON FREDRICK MWANDAGONE | BULOMBORA |
23 | ALEX LEOPOLD ULAYA | BULOMBORA |
24 | SEIF RAMADHANI IDDI | BULOMBORA |
25 | NELSON GERALD MUNYI | BULOMBORA |
26 | FRANK NELSON TITO | BULOMBORA |
27 | NOVATUS JEREMIA MASUNZU | KANEMBWA |
28 | JUVENALI AMEDEUS TARIMO | MAFINGA |
29 | WAISAKA CHACHA KICHELE | MAKUTUPORA |
30 | PIUS SIMON HONGOA | MAKUTUPORA |
31 | MICHAEL ALEX MWAKIHABA | MAKUTUPORA |
32 | WANSAMA KENYUNKO EDWARD | MAKUTUPORA |
33 | HIDAYA YOELI MBWAMBO | MAKUTUPORA |
34 | GETRUDA SIMON YANSEBO | MBWENI |
35 | AZIZI RAMADHANI MNG'ALI | MBWENI |
36 | ANDREW MATHEW MAYUNGU | MBWENI |
37 | BARAKA NGALILWA | MBWENI |
38 | MIDIAN CHARLES MJUNGU | MBWENI |
39 | JOSEPH DAMAS MHAGAMA | MLALE |
40 | HAMISI SAID ONGOLOMA | MLALE |
41 | ELIBARIKI MESIAKI SELEO | MLALE |
42 | ZABRON GEORGE | MLALE |
43 | NYOTA SEBASTIAN LUKUWI | MLALE |
44 | VICENT THEOPHIL SHAGI | MLALE |
45 | AMOS PASCHAEL BINAMUNGU | MSANGE |
46 | FRANK FAUSTUS KAILI | NACHINGWEA |
47 | GLORIUS OBERLIN MASAWE | NACHINGWEA |
48 | WILFRED ASAGWILE MWALINGO | NACHINGWEA |
49 | DAVID MATHIAS KAHYOLO | RWAMKOMA |
50 | EUNICE PEJIWA SIMANDO | RWAMKOMA |
51 | MAKENE ELIAS NYANKORO | RWAMKOMA |
52 | MERINDA ALLOYCE MASIGE | MGULANI |
53 | MARY SOSTENES BUGALAMA | OLJORO |
54 | BERENADETHER ELIZEUS DOMINICK | OLJORO |
55 | JACKSON DEOGRATIUS MICHAEL | MTABILA |
56 | LILIAN DEOGRATIUS NYANYIGE | MARAMBA |
Friday, March 18, 2016
Orodha ya nyongeza ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na jeshi la magereza
Monday, March 14, 2016
Waziri mkuu Kassim Majaliwa ampongeza kamishna jenerali wa magereza kwa namna anavyosimamia utendaji kazi mzuri wa jeshi hilo nchini
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja
akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa Majaliwa(MB) alipotembelea Kambi Maalum ya Mwisa
inayohifadhi Wakimbizi kutoka nchini Burundi leo Machi 14, 2016
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa(MB)akitoa hotuba yake fupi kwa Maafisa na askari wa wa Jeshi
la Magereza(hawapo pichani) kutoka vituo mbalimbali vya Magereza
yaliyopo Mkoa wa Kagera alipotembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa leo
Machi 14, 2016.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mkubwa
hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa(hayupo pichani).
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja
akitoa taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini mbele ya Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(hayupo
pichani).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni akitoa neno
fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kutoa hotuba yake fupi.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, SACP. Omari (aliyesimama kushoto)
taarifa fupi ya Wambizi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa akiongea na Wakimbizi(walioketi chini) katika Kambi ya Mwisa
inayosimamiwa na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Shirika la
kuwahudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR).
Msafara
wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa ukiondoka katika Kambi ya Mwisa iliyopo Mkoani Kagera
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amempongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja kwa utendaji wake mzuri wa kazi kwa namna anavyosimamia kikamilifu utekelezaji wa majukumu wa Jeshi hilo.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu kwenye ziara yake Mkoani Kagera aliyoifanya katika Kambi ya Utenganisho ya Mwisa inayoendeshwa na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR).
"Nampongeza sana Kamishna Jenerali Minja hususani kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuhakikisha kuwa Jeshi la Magereza linaendelea kutekeleza kikamilifu majukumu yake kwa kuzingatia Sheria za Magereza mbali na changamoto kadhaa zinazolikabili Jeshi hilo ikiwemo Msongamano mkubwa uliopo Magerezani." Alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamilia kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazokabili Jeshi hilo ili kuwezesha ufanisi zaidi wa utekelezaji wa majukumu yake.
Awali akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu kwenye ziara yake Mkoani Kagera aliyoifanya katika Kambi ya Utenganisho ya Mwisa, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja alisema kuwa Jshi la Magereza linakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa kiasi fulani zinaathiri utekelezaji wa majukumu yake.
Jenerali Minja alizitaja baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na Msongamano wa wafungwa Magerezani, ufinyu wa bajeti, makazi duni ya Maafisa n askari, uhaba wa vitendea kazi, uhaba na uchakavu wa vyombo vya usafiti na mawasiliano, ukosefu wa pembejeo, ukosefu wa Magereza katika baadhi ya Wilaya mpya zinazoanzishwa kiutawala.
Aidha, Jenerali Minja amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto hizo, Jeshi la Magereza limekuwa likifanya jitihada mbalimbali na za makusudi kwa kufanya maboresho katika maeneo kadhaa ili kujiongezea tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa yupo Mkoani Kagera kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo ambapo katika ziara yake pia ameweza kuitembelea Kambi ya Mwisa inayohifadhi Wakimbizi kutoka nchini Burundi.
(Picha na
Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Sunday, March 13, 2016
Kamishna Jenerali Minja atembelea kambi maalum ya wakimbizi kutoka Burundi inayosimamiwa na jeshi la Magereza pamoja na shamba la mifugo gereza Kitengule, mkoani Kagera
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja akisalimiana na
Mkuu wa Kambi ya Utenganisho Mwisa, SP. S. Lubinza alipotembelea katika
Kambi hiyo Machi 12, 2016 kisha kuongea na Wakimbizi kutoka Burundi
ambao wanazuiliwa katika Kambi hiyo kwa mujibu wa Sheria.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja pamoja na ujumbe
wake aliofuatana nao akikagua sehemu mbalimbali za Kambi hiyo ili kuona
kama zinakidhi viwango vinavyokubalika katika kuwahifadhi Wakimbizi hao
ambao wanahifadhiwa katika Kambi hiyo.
Askari Mlinzi kutoka Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza akiwa timamu
kiulinzi kama anavyoonekana katika eneo lake la kazi ili kuhakikisha
Ulinzi na Usalama wa Kambi hiyo Maalum iliyopo Mkoani Kagera.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja(katikati) akiongea
na Wakimbizi kutoka nchini Burundi(hawapo pichani) ambao wanahifadhiwa
katika Kambi hiyo Maalum kwa sababu za kiusalama.
Sehemu ya kundi la ngo'mbe wa maziwa na nyama wakiwa zizini katika
Shamba la Mifugo linalomilikiwa na Jeshi la Magereza katika Gereza la
Kilimo Kitengule lililopo Mkoani Kagera.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja akikagua ujenzi
unaoendelea wa Jengo la Banda la ndama katika Shamba la Mifugo
linalomilikiwa na Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo Kitengule
lililopo Mkoani Kagera alipotembelea katika ziara yake ya kikazi Machi
12, 2016.
Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Mifugo linalomilikiwa na
Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo Kitengule.
(Picha zote na Lucas
Mboje wa Jeshi la Magereza)
Friday, March 11, 2016
Ziara ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini mkoani Kagera
Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja( wa pili kushoto) akikagua maeneo mbalimbali ya Gereza Bukoba alipofanya ziara ya kikazi leo Machi 11, 2016 (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, SACP. Omari Mtiga (wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza Bukoba, ACP. Benizeth Bisibe.
Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kagera mara baada ya kutembelea Gereza la Wilaya ya Bukoba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella akiongea ofisini kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja na ujumbe wake (hawapo pichani)
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella akiongea ofisini kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja na ujumbe wake kama inavyoonekana katika picha.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Mhe. Sivangilwa Mwangesi Akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja alipomtembelea ofisini kwake
(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Kamishina Jenerali wa Mageraza nchini John Carmir Minja afanya ziara ya kikazi Mkoani Kagera yenye lengo la kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa wa Kagera pamoja na kujionea miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo.
Akiwa Mkoani hapa Kamishna Jenerali Minja alifika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella na kufanya naye mazungumzo kuhusu utendaji kazi na ufanisi wa Jeshi la Magereza Mkoani hapa katika kuimarisha ulinzi na usalama.
Aidha katika mazungumzo hayo walizungumzia changamoto ya msongamano wa Mahabusu katika Gereza la Wilaya ya Muleba ambalo hivi sasa linatumika kuhifadhi Mahabusu wa Wilaya ya Muleba na Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambayo haina Gereza la Wilaya.
Kamishna Jenerali wa Mageraza nchini John Carmir Minja pia alitembelea Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na kufanya mazungumzo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Mhe. Sivangilwa Mwangesi juu ya namna ya kuongeza kasi ya usikilizwaji wa kesi mbalimbali za watuhumiwa ili kuondoa msongamano Magerezani.
Vilevile Kamishna Jenerali Minja alitembelea Gereza la Wilaya la Bukoba na kuongea na wafungwa na Mahabusu wa Gereza hilo pia na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la zahanati ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilishwa ili liweze kutoa huduma za afya kwa wafungwa na watumishi wa Jeshi hilo pamoja na wananchi wanaoishi jirani na zahanati hiyo.
Kamishna Jenerali Minja yupo Mkoani Kagera kwa siku 7 kuanzia tarehe 10 hadi 16 Machi, 2016 ambapo lengo la ziara hiyo ni kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa wa Kagera pamoja na kujionea miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na jeshi hilo.
Thursday, March 10, 2016
Kamishna Jenerali wa Magereza atembelea gereza Biharamulo pamoja na eneo linakojengwa gereza la wiliya ya Chato mkoani Geita
Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP John Casmir Minja akisalimiana na
Mkuu wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza Kamishna Msaidizi wa Magereza, Jaili
Mwamugunda alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya kuanza
ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera ambapo leo Machi 10, 2016 ametembelea
eneo kunakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato lililopo Mkoani Geita
pamoja na Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wengine) ni Maofisa wa Jeshi la
Magereza kutoka Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akifurahia jambo pamoja
na Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Ndomba walipokutana katika Kivuko cha
Busisi kabla ya kuendelea na safari kuekelea Mkoani Kagera(kulia) ni
Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, Goleha Masunzu.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaban Ntarambe(kushoto) akiwa na Kamati
yake ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya wakielekea eneo linakojengwa Gereza
la Wilaya ya Chato mara baada ya Kamishna Jenerali wa Magereza kuwasili
Wilayani Chato kabla ya kuelekea Mkoani Kagera.
Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Omar Mtiga(wa pili kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali wa
Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kulia) nyumba mbili za Askari wa
Jeshi la Magereza ambazo tayari zimekamilika katika eneo linakojengwa
Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wa pili kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya
Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa na
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Chato wakiaangalia
moja ya Bweni la kulala Wafungwa/Mahabusu ambalo tayari limekamilika
katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Kukamilika kwa Gereza hilo kutasaidia kutatua tatizo la Msongamano wa
Wafungwa na Mahabusu katika Magereza ya Biharamulo na Gereza Muleba.
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akisaini katika kitabu
cha Wageni alipotembelea Gereza la Wilaya ya Biharamulo katika ziara
yake ya kikazi leo Machi 10, 2016.
Mkuu wa Gereza la Biharamulo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Gidion
Kakulu akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza maeneo mbalimbali ya
Gereza hilo katika ziara yake ya Kikazi leo Machi 10, 2016. Wengine ni
Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo ambao wameambatana na Kamishna Jenerali
wa Magereza katika ziara yake ya kikazi.
Wednesday, March 9, 2016
Tangazo la kuitwa chuoni
TANGAZO LA KUITWA CHUONI
2. Picha (Passport size) za rangi 5 za hivi karibuni.
Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania Bara anawatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza baada ya Usaili kufanyika katika kambi mbalimbali za JKT. Usaili huu ulihusu vijana waliohitimu Shahada ya Kwanza, Stashahada, Astashahada, Kidato cha Sita na Kidato cha Nne.
Wahusika wote wanatakiwa kuripoti katika Ofisi za Wakuu wa Magereza Mikoa mara wapatapo taarifa hii tayari kwa safari ya kwenda Chuo cha Mafunzo ya Awali kilichopo Kiwira Tukuyu Mkoani Mbeya.
Mafunzo yanategemewa kuanza tarehe 12 Machi, 2016 hivyo mwisho wa kuripoti chuoni ni tarehe 14 Machi, 2016. Yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa tarehe iliyotamkwa kwenye tangazo hili hatapokelewa.
Wahusika wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
1. Walete vyeti halisi vya masomo na vya kuzaliwa, vikiwa na pamoja na nakala 5 za kila cheti.
2. Picha (Passport size) za rangi 5 za hivi karibuni.
3. Chandarua cheupe cha duara ft 31/2, shuka nyeupe mbili, mto wenye foronya nyeupe zisizo na maua/maandishi.
4. Fedha taslimu Tshs.90,000/=.
5. Kalamu za wino, za risasi na madaftari ya kutosha.
6. Cheti cha afya kutoka kwa hospitali ya Serikali.
7. Nguo za kiraia za kutosha sweta, raba (Brown au nyeusi) na soksi
8. Kwa wale wenye kadi za Bima waje nazo na
9. Kila mwanafunzi atajitegemea kwa nauli ya kwenda.
Tangazo hili linapatikana kwenye mbao za matangazo zilizopo Ofisi za Magereza, tovuti ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.go.tz sanjari na blog ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.blogspot.com
Imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza.
SIGNED
Dr. J. A. Malewa - CP
Kny: KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
Subscribe to:
Posts (Atom)