Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja akisalimiana na
Mkuu wa Kambi ya Utenganisho Mwisa, SP. S. Lubinza alipotembelea katika
Kambi hiyo Machi 12, 2016 kisha kuongea na Wakimbizi kutoka Burundi
ambao wanazuiliwa katika Kambi hiyo kwa mujibu wa Sheria.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja pamoja na ujumbe
wake aliofuatana nao akikagua sehemu mbalimbali za Kambi hiyo ili kuona
kama zinakidhi viwango vinavyokubalika katika kuwahifadhi Wakimbizi hao
ambao wanahifadhiwa katika Kambi hiyo.
Askari Mlinzi kutoka Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza akiwa timamu
kiulinzi kama anavyoonekana katika eneo lake la kazi ili kuhakikisha
Ulinzi na Usalama wa Kambi hiyo Maalum iliyopo Mkoani Kagera.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja(katikati) akiongea
na Wakimbizi kutoka nchini Burundi(hawapo pichani) ambao wanahifadhiwa
katika Kambi hiyo Maalum kwa sababu za kiusalama.
Sehemu ya kundi la ngo'mbe wa maziwa na nyama wakiwa zizini katika
Shamba la Mifugo linalomilikiwa na Jeshi la Magereza katika Gereza la
Kilimo Kitengule lililopo Mkoani Kagera.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja akikagua ujenzi
unaoendelea wa Jengo la Banda la ndama katika Shamba la Mifugo
linalomilikiwa na Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo Kitengule
lililopo Mkoani Kagera alipotembelea katika ziara yake ya kikazi Machi
12, 2016.
Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Mifugo linalomilikiwa na
Jeshi la Magereza katika Gereza la Kilimo Kitengule.
(Picha zote na Lucas
Mboje wa Jeshi la Magereza)