Mkuu wa Gereza Tukuyu, Mkoani Mbeya, SSP. Prosper Kinyaga akionesha sehemu ya eneo lenye ekari 26 linaloendesha Kilimo cha chai katika gereza hilo.
Wafungwa wa Gereza Tukuyu, Mkoani Mbeya wakivuna chai katika Shamba la Gereza hilo kama inavyoonekana katika picha.
Muonekano wa baadhi ya mashamba ya Kilimo cha chai katika Gereza Tukuyu. Gereza hilo lilijengwa mwaka 1944 na shughuli zinazofanyika ni Kilimo cha chai, Kilimo cha Migomba, Bustani za mbogamboga pamoja na Utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti na ufugaji wa samaki kwa majaribio(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).