Banner

Banner

Wednesday, January 4, 2017

MASAUNI AFANYA ZIARA MAGEREZA, AAGIZA SARE ZOTE ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA IDARA YA UHAMIAJI KUANZIA SASA ZISHONWE KIWANDA CHA MAGEREZA UKONGA, JIJINI DAR ESA SALAAM

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu, jijini Dar es Salaam wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Jeshi hilo leo. Masauni mara baada ya kumaliza ziara yake aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji nchini, kuanzia sasa sare zote za askari na maafisa wa Idara hizo zitashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza, Julius Chego (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara katika eneo la Ujenzi wa nyumba hizo 320, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo, ambazo Rais Dk. John Magufuli ametoa Shilingi Bilioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Dk Juma Malewa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiiikagua moja ya nyumba za askari wa Jeshi la Magereza zinazojengwa Ukonga, jijini Dar es Salaam. Jumla ya nyumba 320 zinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo mara baada ya Rais Dk John Magufuli kutoa shilingi Bilioni Kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Masauni alifanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo, na alitoa agizo kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Idara ya Uhamiaji, kuhakikisha kuwa, sare za idara hizo kuanzia sasa zitakuwa zinashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga. Mbele kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akitoka katika Jengo la Useremala mara baada ya kukagua mashine mbalimbali zinazotumika kuranda na kuchana mbao kwa ajili ya utengenezaji wa samani katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, na kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiviangalia viti vilivyotengenezwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam, huku Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa akitoa maelezo ya utengenezaji wa viti hivyo. Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho na kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akikiangalia kitanda kilichotengenezwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam, huku Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa (kushoto) akitoa maelezo ya utengenezaji wa kitanda hicho.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikiangalia kikapu kilichoshonwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho na kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani hapo. Watatu kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa.  

Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.