Banner

Banner

Wednesday, May 31, 2017

BODI YA KWANZA YA CHUO CHA TAALUMA YA UREKEBISHAJI TANZANIA YAZINDULIWA

Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba ya ufunguzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza – SACP. Gideon Nkana akitoa historia fupi ya Chuo.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi hiyo wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Dkt. James Jesse akitoa neno la shukrani baada ya hotuba ya Mgeni rasmi.
Wajumbe wa Sekretarieti ya Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania wakitekeleza majukumu yao katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo.
Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kulia) akiteta jambo na baadhi ya Wajumbe wa Bodi kabla ya uzinduzi rasmi uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017.
Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania wakiongozwa na mwenyeji wao Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, SACP. Gideon Nkana(wa kwanza kulia) kutembelea mazingira ya chuo hicho.
 Muonekano wa mbele wa Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania.
Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania. Walioketi kutoka kulia ni SACP. Gideon Nkana, Godfrey Semango na Dkt. Zena Mabeho. Kutoka kushoto ni DCP. Ally Lugendo, Bi. Catherine Jorome na Dkt. James Jesse. Waliosimama(kushoto) ni SACP. Dkt. Kato Rugainunura(katikati) ACP. Charles Novart na wa kwanza kulia ni SACP. Uwesu Ngarama.

(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza)