Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiagana na Kiongozi Mkuu wa kimila kabila la Wasafa lililopo Mkoani Mbeya, Rocket Mwashinga mara baada ya mazungumzo mafupi walipokutana katika viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya, leo Desemba 31, 2017. Kamishna Jenerali wa Magereza nchini yupo Jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambapo hadi jana amefanya ukaguzi katika Magereza ya Ruanda, Kyela, Tukuyu pamoja na Chuo cha Mafunzo ya Magereza, Kiwira kilichopo Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kimila Mkoani Mbeya(kushoto) ni Kiongozi Mkuu wa kimila kabila la Wasafa lililopo Mkoani Mbeya, Rocket Mwashinga(kulia) ni Kiongozi wa Pili wa Wasafa Mkoani Mbeya, George Joto mara baada ya mazungumzo mafupi na Kamishna Jenerali wa Magereza walipokutana katika viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya, leo Desemba 31, 2017
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).