Waziri Kilimo Dk. Charles Tizeba akisalimiana na
Mkuu wa Kilimo,Mifugo na Utunzaji wa Mazingira wa Jeshi la Magereza Kamishna
Msaidizi Mwandamizi Mlasani Deodathy
Kimaro ,katikati yao ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mataka na wa pembeni kwa
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Kimaro ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishna
Msaidizi Shaku Umuya Umba.
Waziri wa Kilimo Dk. Tizeba akiweka
saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kukaribishwa kwenye banda la
Magereza kwenye ufunguzi wa nane nane ambayo inayafanyika Kitaifa
Nyakabindi,Bariadi Mkoani Simiyu.
Sajini Caroline William Mtolela wa
Jeshi la Magereza akimuelimisha Dk. Tizeba jinsi ya kutunza mazingira kwa
kutengeneza mkaa nafuu wa taka ngumu.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Ndugu Adam Malima
akifurahia jambo na Waziri wa Kilimo Dk. Tizeba walipokuwa wakipata maelezo
kwenye banda la uzalishaji uyoga lililo kwenye eneo la Magereza.
Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Hussein
Nyembo akimuelezea Dk. Charles Tizeba uhifadhi bora wa malisho ya mifugo.
Mrakibu Msaidizi wa Magereza Yunge
Saganda akimuonesha na kumuelezea Dk. Charles Tizeba utengenezaji na
upatikanaji wa bidhaa za ngozi katika Jeshi la Magereza, mwenye miwani katikati
yao ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega