Na
Deodatus Kazinja
Wito
umetolewa kwa Asasi mbalimbali za kiraia kujitokeza kushirikiana na Jeshi la
Magereza nchini katika kukabiliana na
baadhi ya changamoto zinazoweza kulikwamisha katika kutoa huduma muhimu za
wafungwa kutokana na ufinyu wa bajeti.
Hayo
yamesemwa leo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Phaustine Kasike
katika hafla ya kupokea msaada wa Kibinadamu uliotolewa na Asasi ya Kidini ya
New Life In Christ iliyofanyika katika
viwanja vya Gereza Kuu Karanga mjini Moshi leo Septemba 8, 2018.
“Ni
ukweli usiopingika kuwa Jeshi la Magereza limekuwa likishindwa kutekeleza kwa
ukamilifu utoaji wa baadhi ya huduma muhimu kwa wafungwa kutokana na ufinyu wa
bajeti” Amesema Kamishna Jenerali Kasike
Na
kuongeza “ natoa wito kwa Asasi nyingine kuiga mfano uliooneshwa na New Life in
Christ na Dorcas Aid International Tanzania zinavyoshirikiana na Jeshi la
Magereza”
Asasi
ya Kidini ya New Life In Christ pamoja
na Dorcas Aid International Tanzania kwa miaka 14 sasa tangu 2005 zimekuwa
zikishirikiana na Jeshi la Magereza kwa kutoa misaada ya Kibinadamu na Kiroho
yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.7.
Kwa
kipindi chote hicho Asasi hizi zimekuwa zimekuwa zikitoa huduma mbalimbali
ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa semina za ushauri pamoja na mafunzo ya ufundi
stadi kwa wafungwa na maafisa wa magereza.
Huduma
nyingine ni kuwa na vituo vidogo vidogo vya kujifunza kufanya jambo ambavyo
tayari linafanyika ndani ya magereza kama vile uokaji mikate, ushonaji na
kudarizi, ushonaji wa viatu, ukinyozi,useremala na uchomeleaji mchanganyiko.
Katika
hafla hiyo Asasi ya Kidini ya New Life In Christ imekabidhi msaada wenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.2. Na kuahidi kuendelea kutoa misaada
ya namna hiyo kwa kadiri Mungu atakavyowajali.
Misaada
ya Kibinadamu iliyotolewa leo imewalenga zaidi wafungwa walioko mkoani
Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Mwanza. Ambapo Kamishna Kasike amewaagiza
wakuu wa magereza yote ambayo vifaa
hivyo vitapelekwa kuhakikisha wanavitunza na kuvitumia kwa uadilifu kama
ilivyokusudiwa.