Na
Shani Mhando, Morogoro
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jinsia katika Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Wazee
na Watoto Bi.Mboni amefurahishwa kuanzishwa
kwa mtandao wa wanawake katika
jeshi a magereza nchini
akizungumza
katika ufunguzi wa mafunzo ya mtandao
huo, uliofanyika katika ukumbi wa Umwema Mkoani Morogoro,Bi Mboni amesema, hii
ni hatua nzuri sana yakupongezwa kwa Jeshi la Magereza kuhakikisha
wanawake katika Nyanja zote wanatumia
fursa mbalimbali zilizopo na zitakazojitokeza ndani ya Jeshi na Nje ya Jeshi
ili kujipatia mafanikio.
aliongeza
kuwa msingi wa kuwepo kwa mitandao ya wanawake ni nchini ni kuwawezesha na
kuwajengea uwezo wanawake katika Nyanja
za kiuchumi,mafunzo,ajira,uongozi na maamuzi ili kuweza kutimiza majukumu yao
bila kubaguliwa jinsia zao.
“Ni
matarajio yangu kuwa kuanzishwa kwa mtandao huu Jeshi la magereza litazingatia
miongozo na kanuni mbalimbali zilizotolewa na serikali kuhakikisha katika
maeneo yote yenye changamoto za usawa wa kijinsia mwanamke awezeshwe ili aweze
kukabilina nazo,”alisema Bi Monica
Aidha
Bi Mboni amewaasa washiriki wa mafunzo kuzingatia yote watakayofundishwa katika
mafunzo hayo ili wakawe wawakilishi wazuri kwa askari wote wa kike katika Jeshi
la Magereza ili kuwajengea uwezo,kukuza uelewa na kuwaunganisha waweze kufanya
kazi kw ufanisi zaidi.
“Jukumu
mlilopewa na Jeshi la Magereza la uelimshaji ni jukumu muhimu sana katika
ustawi wa mtandao wa wanawake ndani ya Jeshi la Magereza, ninahakika,mafunzo
mtakayoyapata yatawaongezea uwezo wa kutekeleza jukumu hili muhimu na kuleta
ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya mtando ndani Jeshi,”alisema Bi Mboni
kwa
upande wa Mkuu wa dawati la Jinsia Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Bertha
Joseph Minde amesema kuanzishwa kwa mtandao wa wanawake magereza kumewawezesha
wanawake Kushika nafasi za juu za
uongozi katika Jeshi kama kamishna mmoja,kamshna msaidizi mwandamizi mmoja na
makamishn wasaidizi 6 ingawa bado kuna upungufu mkubwa wa kinamama katika
nafasi za juu za uongozi.
naye
msemaji wa Jeshi la Magereza Mrakibu mwandamizi Amina kavirondo amemuomba
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo Bi
Mboni kuwashika mkono mtandao wa wanawake
Magereza ili kuweza kufikia malengo waliyokusudia
Aidha
kamishna msaidizi mwandamizi wa mkoa wa morogoro (RPO) Ismail T.Mlawa aliwapongeza wanawake wa Jeshi
la Magereza kwa kuanzisha mtandao wa wanawake ambapo utawawezesha kupambania
haki zao
mtandao wa wanawake katika Jeshi la magereza
ulianzishwa rasmi tarehe7 Desemba,2018 baada ya mkutano wa SADC uliofanyika
Dec.2011 nchini Birchhood Johanesburg Africa ya Kusini ambapo katika kikao hicho
wazo la mtandao wa wanawake lilirasimishwa na kuwekewa mikakati(the idea of
women network consolidation and road map drawn)