Banner

Banner

Friday, February 20, 2015

Asasi ya "AIDS-free" kusaidia mapambano dhidi ya ukimwi ndani ya jeshi la Magereza

 Mkurugenzi wa Mradi wa "AIDS free", Bw. Samson Kironde(wa pili kushoto) akitoa maelezo mafupi namna mradi huo utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza na Polisi katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza leo februari 20, 2015(wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Operesheni na Fedha, Bw. Mike Hames(wa kwanza kushoto) ni Afisa Mwandamizi anayeshughulikia masuala ya UKIMWI kutoka USAID, Bw. Erick Mlang'ha.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisisitiza jambo katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Polisi na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa "AIDS - free" utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioshriki katika mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa "AIDS - free" unaotarajiwa kutekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gedion Nkana(wa kwanza kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja.
Maofisa Wasimamizi wa Sekta ya Afya kutoka Jeshi la Polisi wakifuatilia mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa "AIDS - free"(wa kwanza kushoto) ni Dkt. Nyanda Lushina(katikati) ni Mrakibu wa Polisi, Husein Yahya.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(meza kuu) akiongoza mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa "AIDS - free" utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Tuesday, February 17, 2015

Waziri wa katiba na sheria atembelea makao makuu ya jeshi la magereza, jijini Dar

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akimkaribisha Ofsini kwake Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo februari 17, 2015, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiendelea na mazungumzo na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro(hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo februari 17, 2015, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo februari 17, 2015, Jijini Dar es Salaam.

Thursday, February 5, 2015

Kikao cha kwanza cha bodi ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji gereza Kigongoni-Bagamoyo kati ya shirika la Magereza na kampuni ya Tarbim chafanyika leo mjini Bagamoyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu akitoa maelezo mafupi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo(kushoto) ni Mjumbe wa Bodi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Green Park iliyoko Bagamoyo.
Wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji kutoka Jeshi la Magereza wakisikiliza maelezo ya utambulisho kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim Bw Baddal Calikusu (hayupo pichani)

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (aliyesimama) akitoa utambulisho kwa wajumbe wapya wa Bodi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo .
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana akiwa na Wajumbe wengine wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni wakikagua eneo la Mradi utakapotekelezwa.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni mara baada ya Kikao cha kwanza kilichofanyika katika Hoteli ya Green Park iliyopo Mjini Bagamoyo (wa kwanza kulia) ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana (wa tatu kulia) ni Mjumbe wa Bodi, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Masunga.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)