Banner

Banner

Friday, September 4, 2015

Kamishna wa sheria na uendeshaji wa magereza afunga rasmi kongamano la wasaidizi wa kisheria magerezani mkoani Morogoro

Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba kwa Maofisa Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwenye hafla ya ufungaji wa Kongamano la Wasaidizi wa Sheria lililofadhiliwa na Shirika la Envirocare ambapo Kongamano hilo limefanyika kwa siku tatu kuanzia Septemba 2, 2015 Mkoani Morogoro.
Washiriki wa Kongamano hilo ambao ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa Mitano Tanzania Bara(Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Morogoro) wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji wa Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema akitoa neno la shukrani kwa Washiriki kabla ya kumkaribisha Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza kufunga Kongamano hilo.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akiwa ameongozana na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(kushoto) tayari kwa ufungaji rasmi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria ambalo limefanyika Mkoani Morogoro kuanzia Septemba 02 - 04, 2015

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Thursday, September 3, 2015

Jeshi la Magereza nchini kushirikiana na asasi za kiraia katika kupunguza msongamano magerezani

Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kutoka Magereza Mkoani tanga wakiendelea na majadiliano katika Kongamano hilo linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku tatu.

Na, Lucas Mboje, Morogoro

Jeshi la Magereza nchini limeahidi kuendelea kushirikiana na Asasi ya Envirocare katika kuimarisha Madawati ya Msaada wa Kisheria Magerezani ili kuleta tija katika utatuzi wa changamoto ya Msongamano wa Mahabusu inayolikabili Jeshi hilo.

Kauli hiyo imetolewa jana Mkoani Morogoro na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja alipokuwa Mgeni rasmi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria Magerezani na Mahabusi za Watoto.

Jenerali Minja amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukulia kwa uzito stahiki suala la Msongamano wa Mahabusu Magerezani ikiwemo kushirikiana na Wadau wa Haki Jinai katika kupunguza changamoto ya Msongamano wa Mahabusu Magerezani.

"Napenda kutoa rai kwa Asasi zingine zenye malengo yanayofanana na Asasi hii nazikaribisha kuja kufanya kazi na Jeshi la Magereza kwani mwelekeo wa Jeshi kwa sasa ni Urekebishaji wa Wafungwa(From Prisons to Corrections) ambapo Jeshi la Magereza watafanya kazi kwa karibu na Asasi za Kiraia na Jamii kwa ujumla". Alisema Jenerali Minja.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Envirocare, Bi. Loyce Lema amesema kuwa imekuwa ni faraja kwao kupata ushirikiano kama huo kutoka Jeshi la Magereza kwani umewezesha kutekelezwa kwa mradi huo wa kutoa Msaada wa Kisheria kwa Mahabusu waliopo Magerezani kwa matokeo chanya kwa muda mufupi.

Bi. Lema alisema kuwa mradi huo umetekelezwa kwa miaka mitatu(2012 - 2015) na umetekelezwa kwenye Magereza 20 na Mahabusu 04 za Watoto katika Mikoa 05 ambayo ni Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam.

Asasi ya Envirocare kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza ilifanya utafiti wa awali wa kuangalia hali halisi ya Msongamano katika Magereza yaliyopo katika Mikoa mitano ya mradi. Matokeo ya jumla ya utafiti huo yalionesha kuwa kuna tatizo kubwa la Msongamano ambao unasababishwa na idadi kubwa ya Mahabusu katika Magereza ya Mikoa hiyo.

Wednesday, September 2, 2015

Kamishna Jenerali wa Magereza afungua rasmi kongamano la wasaidizi wa kisheria magerezani mkoani Morogoro

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba kwa Maofisa Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwenye ufunguzi wa Kongamano la Wasaidizi wa Sheria lililofadhiliwa na Shirika la Envirocare ambapo Kongamano hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 2, 2015 Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo ambao ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa Mitano Tanzania Bara(Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Morogoro) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani).
Meza Kuu wakimsikiliza Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani - Jeshi la Polisi, Kamisheni ya Upelelezi, Mrakibu wa Polisi Emmy Mkonyi(hayupo pichani). Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Bw. Joseph Ndunguru(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema akitoa maelezo mafupi ya lengo la Kongamano hilo ambalo ni kutoa msaada wa Kisheria Magerezani ili kupunguza Msongamano Magerezani.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza baada ya kukabidhi cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwa mmoja wa Washiriki wa Kongamano hilo linalofanyika Mkoani Morogoro.
Mwandishi wa Habari wa ITV, Bi. Devotha Minja akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja mara baada ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria katika Viwanja vya Ukumbi wa CCT uliopo Mkoani Morogoro(wa pili kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(kulia) ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Jeshi la Polisi, Mrakibu wa Polisi Emmy Mkonyi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) walioketi akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria kutoka Mikoa Mitano ya Magereza Tanzania Bara(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato Rugainunula(wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Joseph Ndunguru(wa kwanza kushoto) ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Jeshi la Polisi, Mrakibu wa Polisi, Emmy Mkonyi(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).