Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba
kwa Maofisa Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwenye ufunguzi wa
Kongamano la Wasaidizi wa Sheria lililofadhiliwa na Shirika la
Envirocare ambapo Kongamano hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia leo
Septemba 2, 2015 Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo ambao ni Maofisa wa Jeshi la
Magereza kutoka Mikoa Mitano Tanzania Bara(Dar es Salaam, Tanga, Arusha,
Kilimanjaro na Morogoro) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi
ambaye ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir
Minja(hayupo pichani).
Meza Kuu wakimsikiliza Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani -
Jeshi la Polisi, Kamisheni ya Upelelezi, Mrakibu wa Polisi Emmy
Mkonyi(hayupo pichani). Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria
kwa Umma kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Bw. Joseph
Ndunguru(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi.
Loyce Lema(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John
Casmir Minja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema akitoa
maelezo mafupi ya lengo la Kongamano hilo ambalo ni kutoa msaada wa
Kisheria Magerezani ili kupunguza Msongamano Magerezani.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza
baada ya kukabidhi cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Wasaidizi wa Kisheria
Magerezani kwa mmoja wa Washiriki wa Kongamano hilo linalofanyika Mkoani
Morogoro.
Mwandishi wa Habari wa ITV, Bi. Devotha Minja akiteta jambo na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja mara baada ya ufunguzi
rasmi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria katika Viwanja vya Ukumbi wa
CCT uliopo Mkoani Morogoro(wa pili kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(kulia) ni Mwakilishi kutoka Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Jeshi la Polisi, Mrakibu wa Polisi Emmy
Mkonyi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati)
walioketi akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kongamano la
Wasaidizi wa Kisheria kutoka Mikoa Mitano ya Magereza Tanzania Bara(wa
kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato Rugainunula(wa pili kulia) ni
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria,
Bw. Joseph Ndunguru(wa kwanza kushoto) ni Mwakilishi kutoka Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi - Jeshi la Polisi, Mrakibu wa Polisi, Emmy
Mkonyi(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare,
Bi. Loyce Lema(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).