Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(wa
pili kushoto)akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Huduma za
Magereza Duty free shop Mkoani Arusha leo Septemba 18, 2015 katika
Viwanja vya Gereza Kuu Arusha(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Dar Smart LTD, Bw. Mohamed Panjwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak
Abdulwakil(kulia)akisoma jiwe la Msingi kwenye hafla ya uzinduzi wa Duty
free shop ya Magereza Mkoani Arusha(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa
Magereza, John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa
maelezo mafupi wakati wa kumkaribisha Mgeni rasmi katika hafla ya
uzinduzi wa Huduma za Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha.
Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Magereza mbalimbali yaliyopo Mkoani
Arusha wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbaraka Abdulwakil(hayupo pichani).
Bidhaa za majumbani zinazopatikana katika Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak
Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na
Usalama Mkoani Arusha waliosimama mara tu baada ya kuzindua Huduma za
Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha(wa pili kushoto) ni Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mkuu wa
Magereza Mkoani Arusha, SACP. Hamis Nkubasi(wa kwanza kushoto) ni Mkuu
wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, SACP. Venant Kayombo(wa kwanza kulia) ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Mart LTD, Bw. Mohamed Panjwani
Na Lucas Mboje, Arusha
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil
amepongeza kasi ya Utendaji kazi wa Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, John Casmir Minja pamoja na Uongozi wote wa Jeshi hilo kwa
kutekeleza kwa mafanikio makubwa mpango wa Serikali ya Awamu ya Nne wa
kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa Maafisa, askari
Magereza na familia zao katika maeneo yao ya kazi hususani huduma za
"Duty free shops".
Mhe. Mbarak
Abdulwakil ameyasema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa "Duty free shop"ya
Magereza Mkoani Arusha iliyofanyika leo Septemba 18, 2015 katika
Viwanja vya Gereza Kuu Arusha ambapo baadhi ya Viongozi mbalimbali wa
Kiserikali na Binafsi wa Mkoa wa Arusha walihudhuria hafla hiyo.
"Nampongeza
kwa dhati Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja kwa jitihada
hizi ambapo matunda yake yanaonekana na amethibitisha kwamba azma ya
kusambaza huduma hii nchi nzima ipo pale pale na jitihada zinaonekana".
Alisema Abdulwakil.
Ameongeza kuwa lengo la Mpango huu ni kuhakikisha kuwa ustawi wa maisha ya Maafisa na Askari wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama unatekelezwa ipasavyo kwa kuwapatia bidhaa zenye bei nafuu ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
Aidha, Mhe. Abdulwakil amewaasa Maafisa na askari watakaotumia huduma husika kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu pamoja na maadili ya uendeshaji wa maduka hayo ili kuhakikisha kuwa adhima ya Serikali ya kuwapunguzia makali ya maisha Maafisa, askari pamoja na familia zao wananufaika ipasavyo na si vinginevyo.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi,Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja alisema kuwa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Kampuni ya Dar Mart LTD limeazimia kusambaza huduma za Duty Free Shop nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa Maafisa na askari.
Kamishna Jenerali Minja alimhakikishia Mgeni rasmi kuwa maduka hayo yataendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za "Duty Free Shop" na akasema kuwa hata sita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa na askari watakao kwenda kinyume na uendeshaji wa huduma hizo.
Hivi sasa Jeshi la Magereza limefanikiwa kuzindua jumla ya "Duty Free Shops" tisa(09) ikiwemo Gereza Kuu Ukonga na Keko - Dar es Salaam, Gereza Isanga - Dodoma, Gereza Kuu Karanga - Moshi, Gereza Butimba - Mwanza, Gereza Ruanda - Mbeya, Gereza Lilungu - Mtwara, Gereza Uyui - Tabora, Chuo KPF - Morogoro na duka la tisa(09) ni Gereza Kuu Arusha.

(Picha zote na
Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).