Banner

Banner

Friday, January 13, 2017

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MWIGULU NCHEMBA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA KIKOSI MAALUM CHA MAGEREZA JIJINI DAR

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb)  akipokea Salaam ya heshima kutoka Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11. Hafla ya hiyo imefanyika leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Dkt. Juma Malewa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akikagua Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na Askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kama inavyoonekana katika picha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akimtunuku cheti cha sifa Mmoja wa askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 ambapo Mafunzo hayo yamefungwa rasmi leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akimvisha nembo ya kijani Mmoja wa askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kwa niaba ya wahitimu wenzake. Mafunzo hayo Maalum yamefungwa rasmi leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kabla ya kuyafunga rasmi leo Januari 13, 2017.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo hayo.
Askari Wahitimu wa Mafunzo hayo Maalum wakionesha umahiri wao wa kuvuka vikwazo mbalimbali kwa kutumia kamba kama inavyoonekana katika picha.
Onesho Maalum la Ukakamavu na ujasiri kama inavyoonekana katika picha Askari wa Kikosi Maalum akihimiri kipigo cha nyundo katika mwili wake kwa ujasiri wa hali ya juu.
Askari Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 wakiingia uwanjani kwa ajili ya kutoa maonesho mbalimbali ya Ukakamavu na ujasiri.
Wahitimu wa Mafunzo Maalum wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha

(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Saturday, January 7, 2017

KAIMU KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT JUMA MALEWA AFANYA MABADILIKO YA UONGOZI KWA MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA

Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Ally Malewa(pichani) amefanya Mabadiliko ya Uongozi kwa baadhi ya Wakuu wa Magereza Mikoa na vituo mbalimbali hapa nchini.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Katos Rugainunura amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza sehemu ya Utawala na nafasi yake inakaimiwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Mzee Nyamka aliyekuwa Mkuu wa Utawala Magereza Mkoani Morogoro. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Antonino Kilumbi  aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma amehamishwa kwenda Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Julius Sang’udi aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya.

Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Anderson Kamtiaro anaenda kuwa Afisa Mnadhimu Magereza Mkoani Arusha na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Hassan Mkwiche ambaye alikuwa ni Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Gereza Same Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Evarist Katego anakwenda kuwa Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Uwesu Ngarama amehamishiwa Makao Makuu kuwa Boharia Mkuu wa Jeshi na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mipango wa Jeshi ACP Athuman Kitiku.  

Aidha,  aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoani Mtwara,  Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Musa Kaswaka anakwenda Makao Makuu Kitengo cha Ukaguzi  na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Ismail Mlawa aliyekuwa Mkuu wa Kiwanda cha Samani Gereza Kuu Ukonga. Aliyekuwa Afisa Mdhibiti wa Fedha wa Jeshi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Gideon Nkana anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga, Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Chacha Jakson.

Wengine ni pamoja na aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Mbeya ACP Kijida Mwakingi anakaimu nafasi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Abdalah Misanga anayetoka Gereza Mgumu kwenda kuwa Mkuu wa Gereza Msalato, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP  John Itambu anayetoka Gereza Kilosa kwenda kuwa Mkuu wa Kiwanda cha Samani Gereza Kuu Ukonga.

Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Erasmus Kundy anayetoka Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga kwenda Makao Makuu Kitengo cha Habari, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Julius Ntambala aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi Makao Makuu anabakia Makao Makuu Kitengo cha ujenzi kuwa Msaidizi wa Mkuu wa Kitengo, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Sylivester Mrema  anayetoka Gereza Idete kwenda Gereza Ubena kuwa Mkuu wa Gereza.

Aliyekuwa Mkuu wa Gereza Ubena Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Shaba Zephania anakwenda Magereza Mkoa wa Pwani kuwa Afisa Mnadhimu, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Solomon Urio anayetoka Makao Makuu kwenda Magereza Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Afisa Mnadhimu pamoja na aliyekuwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP George Kiria amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Uhasibu .

Mabadiliko hayo ni ya kawaida na yanalenga kuboresha utendaji kazi na ufanisi wa Jeshi la Magereza.

Imetolewa na:

Lucas Mboje - ASP
Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza
Makao Makuu ya Magereza Tanzania Bara
07 Januari, 2017.

Wednesday, January 4, 2017

MASAUNI AFANYA ZIARA MAGEREZA, AAGIZA SARE ZOTE ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA IDARA YA UHAMIAJI KUANZIA SASA ZISHONWE KIWANDA CHA MAGEREZA UKONGA, JIJINI DAR ESA SALAAM

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu, jijini Dar es Salaam wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Jeshi hilo leo. Masauni mara baada ya kumaliza ziara yake aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji nchini, kuanzia sasa sare zote za askari na maafisa wa Idara hizo zitashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza, Julius Chego (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara katika eneo la Ujenzi wa nyumba hizo 320, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo, ambazo Rais Dk. John Magufuli ametoa Shilingi Bilioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Dk Juma Malewa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiiikagua moja ya nyumba za askari wa Jeshi la Magereza zinazojengwa Ukonga, jijini Dar es Salaam. Jumla ya nyumba 320 zinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo mara baada ya Rais Dk John Magufuli kutoa shilingi Bilioni Kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo. Masauni alifanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo, na alitoa agizo kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Idara ya Uhamiaji, kuhakikisha kuwa, sare za idara hizo kuanzia sasa zitakuwa zinashonwa katika Kiwanda cha Magereza, Ukonga. Mbele kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akitoka katika Jengo la Useremala mara baada ya kukagua mashine mbalimbali zinazotumika kuranda na kuchana mbao kwa ajili ya utengenezaji wa samani katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, na kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiviangalia viti vilivyotengenezwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam, huku Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa akitoa maelezo ya utengenezaji wa viti hivyo. Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho na kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akikiangalia kitanda kilichotengenezwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam, huku Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa (kushoto) akitoa maelezo ya utengenezaji wa kitanda hicho.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikiangalia kikapu kilichoshonwa na wafungwa katika Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Masauni alifanya ziara katika kiwanda hicho na kujionea vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na wafungwa kiwandani hapo. Watatu kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk Juma Malewa, kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho, Ismail Mlawa.  

Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.