Banner

Banner

Thursday, November 15, 2018

ZIARA YA CGP KASIKE GEREZA LA WILAYA MAKETE, MKOANI JOMBE



Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike akizungumza jambo alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya Makete Novemba 14, 2018. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
Baadhi ya Askari wa kike wa Jeshi la Magereza wakiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ambapo askari hao wamempongeza Mkuu wa Jeshi hilo kwa uamuzi wake wa kutembelea magereza mbalimbali hapa nchini.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike akiwasili Gereza Makete tayari kwa ziara yake ya kikazi Mkoani Njombe, Novemba 14,  2018.

 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua maandalizi ya mashamba ya kilimo cha mahindi katika eneo la Gereza Ludewa mapema leo asbuhi Novemba 14, 2018  kabla ya kuelekea Gereza Makete kuendelea na ziara yake ya kikazi.
Mkuu wa Gereza Makete, SP. Aloyce Kayera(kushoto) akisoma taarifa ya Gereza mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(kulia) alipotembelea gereza hilo leo Novemba 14, 2018.
. Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Veronica Kessy akiagana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya Makete.


Wednesday, November 14, 2018

GEREZA LUDEWA KUPATIWA TREKTA ILI KUONGEZA UZALISHAJI WA CHAKULA CHA WAFUNGWA


Na Lucas Mboje, Ludewa

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ameahidi kulipatia trekta moja Gereza la Kilimo Ludewa ili kuongeza uzalishaji wa chakula cha wafungwa.

Kamishna Jenerali Kasike ametoa ahadi hiyo leo wakati akizungumza na uongozi wa Gereza hilo baada ya kuwasili Wilayani Ludewa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa Jeshi hilo.

Amesema kuwa Gereza Ludewa ni miongoni mwa magereza 13 ambayo tayari yameainishwa katika mpango mkakati wa Jeshi la Magereza katika kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa waliopo magerezani hivyo lazima liwezeshwe zana za kilimo.

 “Nafahamu kuwa trekta lililopo hapa Gereza Ludewa ni la muda mrefu na ni chakavu, hivyo nitawapatieni trekta jipya ili muweze kuongeza uzalishaji wa chakula cha wafungwa”. Alisema Jenerali Kasike.

Pia, Kamishna Jenerali Kasike amehimiza uongozi wa Gereza hilo kuzingatia suala zima la uadilifu na amewataka kujiepushe na vitendo vyote vya ubadhilifu wa mali za umma.

Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza hilo, SSP. Akley Mkude amesema kuwa  katika msimu wa Kilimo wa mwaka 2017/2018 gereza hilo lililima ekari 200 za mahindi na kufanikiwa kuvuna gunia zaidi ya 1700 ambazo zitatumika kulisha magereza yote ya Mkoa wa Njombe na Iringa.

Aidha, ameongeza kuwa  malengo ya msimu huu wa mwaka 2018/2019 ni kulima ekari 700 za mahindi, ekari 40 za maharage, ekari 30 za alizaeti pamoja na bustani ekari 5 za mbogamboga.

Gereza Ludewa lina eneo lenye ukubwa wa ekari 3500, Gereza hilo linajishughulisha na kilimo cha mahindi, maharage, alizeti pamoja na bustani za mbogamboga. Pia, linajishughulisha na miradi ya ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kuku wa kienyeji pamoja na uhifadhi wa mazingira.


Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike akisalimiana na Maofisa na askari wa Gereza Ludewa alipowasili kuendelea na ziara yake ya kikazi ya kutembelea magereza mbalimbali Mkoani Njombe,  Novemba 13, 2018.

Mkuu wa Gereza Ludewa, SSP. Akley Mkude(kushoto) akimweleza jambo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(kulia) alipotembelea gereza hilo  Novemba 13, 2018. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike akipanda mti wa mparachichi katika Kambi ya Jeshi la Magereza ya Kidewa iliyopo Mkoani Njombe kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Gereza Ludewa, Novemba 13, 2018.
Ghala la kuhifadhia mahindi yanayozalishwa katika Gereza Ludewa.

Baadhi ya Askari wa Gereza la Wilaya Ludewa  wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(hayupo pichani).

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Andrea Tsere(wa tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Ludewa( Picha na Jeshi la Magereza).

Monday, November 12, 2018

WAKUU WA MAGEREZA NCHINI WATAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA UTATUZI WA NYUMBA ZA ASKARI


Na Lucas Mboje, Njombe

WAKUU wa Magereza yote nchini wametakiwa kuwa wabunifu ili kutatua changamoto ya uhaba wa makazi ya askari kwa kutumia nguvukazi ya wafungwa na rasilimali nyinginezo zilizopo katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa leo Novemba 12, 2018 na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua magereza yote ya Mkoa wa Njombe ambayo yanaendeshwa na Jeshi hilo.

Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa lazima wakuu wa magereza wawe wabunifu katika kutatua tatizo hilo la uhaba wa nyumba kwani Jeshi hilo linazo fursa nyingi ikiwemo nguvu kazi ya wafungwa.

“Mkoa wa Njombe na mingineyo nchini haipo sababu ya kuwa na tatizo la uhaba wa nyumba za askari kwani kuna fursa ya kutosha ya kufyatua tofali za kuchoma  kwa kuwatumia wafungwa ili kumaliza tatizo hili nchini”. Amesisitiza Jenerali Kasike.

Aidha, Kamishna Jenerali Kasike amewataka mafisa na askari wote kuendelea kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, sheria na kanuni mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.

Awali, akisoma taarifa ya Gereza la Wilaya Njombe, Mkuu wa Gereza hilo, SP. Charls Mihinga amesema kuwa  tayari wameanzisha mradi wa ufyatuaji wa tofali za kuchoma katika kambi ya mdandu ili kumaliza tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi wa gereza hilo.

“Katika msimu huu tumeweza kufyatua tofali kubwa zipatazo 30,000 ambazo tayari zimeshachomwa, tofali hizi zitatumika katika ujenzi wa nyumba za askari pamoja na ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Magereza Mkoani Njombe”. Alisema SP. Mihinga.

Pia, ameongeza kuwa  malengo ya baadaye ni kuifanya kambi hiyo ya Gereza Njombe kuwa na taswira ya uzalishaji wa matofali kwa wingi kwa ajili ya kufanya biashara na hivyo kuongeza maduhuri serikalini.

Jeshi la Magereza linakabiliwa na uhaba wa nyumba za kuishi za Maafisa na askari hapa nchini, mkakati uliopo hivi sasa chini ya uongozi wa Kamishna Jenerali wa Magereza ni kuhakikisha kuwa tatizo hilo linatatulika kwa kutumia njia ya ubunifu pamoja na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Jeshi hilo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoani Njombe Bw. Erick Shitindi akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike walipokutana  Mkoani Njombe alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Njombe, leo Novemba 12,  2018.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe wakimsikiliza  Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(hayupo pichani) alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani humo.
Baadhi ya Askari wa Gereza la Wilaya Njombe  wakifuatilia maelekezo katika Baraza lililoongozwa na  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ambapo askari hao wameelezea changamoto zao kiutendaji leo Novemba 12, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na askari wa Gereza Njombe.

Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(wa kwanza kulia) akizungumza jambo alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.

Mkuu wa Gereza Njombe, SP. Charles Mihinga(kushoto) akimtembeza Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(kulia) alipotembelea gereza hilo leo Novemba 12, 2018.( Picha na Jeshi la Magereza)