Banner

Banner

Wednesday, February 5, 2020

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, SULEIMAN MZEE AKAGUA USIMIKAJI WA MIUNDOMBINU YA MAJI KATIKA MAJENGO YA MAKAZI YA MAAFISA NA ASKARI MAGEREZA, UKONGA DSM

Kamishna  Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee akisalimiana na Mkuu wa Kiwanda cha Samani cha Gereza Kuu Ukonga, ACP. John Itambu mapema leo alipokagua zoezi la uwekaji miundombinu ya maji katika majengo ya makazi ya Maafisa na askari Magereza, Ukonga Dar es Salaam kabla ya kutembelea eneo la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi hilo.

Mkuu wa Magereza Mkoani Dar es Salaam, SACP. Julius Ntambala(kushoto) akitoa taarifa fupi kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee(wa pili toka kulia) mapema leo alipokagua zoezi la uwekaji miundombinu ya maji katika majengo ya makazi ya Maafisa na askari Magereza, Ukonga Dar es Salaam kabla ya kutembelea eneo la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi hilo.

 Moja ya majengo ya makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza yaliyopo Ukonga Dar es Salaam ambayo yamekabidhiwa hivi karibuni na Rais Magufuli.

Mkuu wa Magereza Mkoani Dar es Salaam, SACP. Julius Ntambala akitoa taarifa fupi kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee(wa pili toka kulia) mapema leo alipokagua zoezi la uwekaji miundombinu ya maji katika majengo ya makazi ya Maafisa na askari Magereza, Ukonga Dar es Salaam kabla ya kutembelea eneo la ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi hilo (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Tuesday, February 4, 2020

NIPENI USHIRIKIANO - KAMISHNA JENERALI MPYA WA MAGEREZA, SULEIMAN MZEE

Na ASP Lucas Mboje, DSM
KAMISHNA Jenerali mpya wa Magereza nchini, Suleiman Mzee (pichani) amewataka Maofisa na askari wote wa Jeshi la Magereza kumpa ushirikiano katika uongozi wake ili aweze kusimamia vyema maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Jeshi hilo ikiwemo jukukumu la kujitegemea kwa chakula cha wafungwa magerezani.
Akizungumza na Maofisa, askari na watumishi raia wa Jeshi hilo katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Magereza, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Suleiman Mzee amesema kuwa anayomatarajio makubwa ya kuhakikisha kuwa Jeshi la Magereza linakuwa na miradi mingi ya uzalishaji mali ili kuwezesha kujitegemea badala ya kutegemea bajeti kuu ya Serikali.
“Ni lazima tuzalishe kwa wingi na kila gereza lizalishe kulingana na fursa zilizopo ikiwa tunataka kujiwekea mazingira ya kuaminika. Pia, tuhakikishe kuwa utaalam wetu katika nyanja mbalimbali lazima uwe na manufaa Jeshini”, amesisitiza Jenerali Mzee.
Aidha, Kamishna Jenerali Mzee ameongeza kuwa ni vyema maofisa na askari wa Jeshi hilo wakazingatia utii, uaminifu pamoja na uhodari katika kazi ili kuyafikia matarajio hayo makubwa ndani ya Jeshi.
“Mkizingatia utii, uaminifu pamoja na uhadari katika kazi naamini matokeo chanya yataonekana katika muda mfupi kwani upo uwezekano wa kufanya mambo makubwa ambayo yataliletea heshima na sifa Jeshi letu la Magereza”, amesema Jenerali Mzee.
Kuhusu mafunzo mbalimbali kwa maafisa na askari, amesema kuwa atapitia mitaala ya mafunzo ili kuona kama inaendana na mazingira yaliyopo pamoja na kuifanyia maboresho mbalimbali kwani mafunzo ni nguzo muhimu katika kujenga nidhamu kwa maafisa na askari.
Kwa upande wake aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(sasa Balozi Mteule) alimpongeza Jenerali Mzee kwa kuteuliwa na Rais kushika nafasi hiyo na alibainisha baadhi ya changamoto ambazo zinalikabili Jeshi hilo ikiwemo uchakavu wa makazi ya askari.
“Nafurahi kuwa naliacha Jeshi la Magereza likiwa na nidhamu ya hali ya juu pamoja na kuwa na baadhi ya changamoto mbalimbali ikiwemo makazi duni ya askari, naamini changamoto hizo utazifanyia kazi kwani tayari tulikwishaanza kuchukua hatua”, amesema Mhe. Balozi Kasike.
Jeshi la Magereza linamiliki ardhi yenye ukubwa wa ekari 326,205 Tanzania Bara, kati ya hizo ekari 151,350 zinafaa kwa shughuli za kilimo na mifugo. Eneo linalotumika kwa shughuli za kilimo kwa sasa ni ekari 20,580 pekee sawa na asilimia 13.60 ya eneo linalofaa kwa shughuli za kilimo. Jeshi hilo likijipanga kimkakati linaweza kujilisha, kuongeza pato serikalini pamoja na kufanya mapinduzi makubwa ya kilimo hapa nchini.

MAPOKEZI YA KAMISHNA JENERALI MPYA WA MAGEREZA OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA MAGEREZA, JIJINI DAR

Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akipokea salaam ya heshima toka  Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kwa ajili yake kwa heshima katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Magereza, Jijini             Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali  mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake kwa heshima kama inavyoonekana katika picha.

Kamishna Jenerali  mpya wa Magereza, Suleiman Mzee  akisalimiana na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (sasa Balozi mteule) alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo baada ya kuapishwa rasmi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020. Kulia ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Uwesu Ngarama.

Kamishna Jenerali  mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akifanya mahojiano maalum na wanahabari baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali  mpya wa Magereza, Suleiman Mzee akiongea na Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020.

Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali mpya wa Ma gereza, Suleiman Mzee mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 3, 2020                         (Picha zote na Jeshi la Magereza).