Banner

Banner

Sunday, November 18, 2018

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NDANI, MEJA JENERALI JACOB KINGU AKAGUA MABORESHO YA KIWANDA CHA VIATU GEREZA KUU KARANGA MOSHI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Jacob Kingu akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuwasili katika ziara Maalum ya kukagua maboresho mbalimbali katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi jana  Novemba 17, 2018. Kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu(meza kuu) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkuu wa Kiwanda hicho, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Hamis Nyaku(aliyesimama). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike wakiangalia Buti za aina mbalimbali za Jeshi zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi.
Sehemu ya viatu aina mbalimbali ikiwemo viatu vya maafisa na Buti za Jeshi zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi kwa ajili ya Jeshi la Polisi nchini. Jeshi la Polisi limetengenezewa viatu aina ya buti pea elfu kumi (10,000) na pea elfu tano (5,000) za viatu vya maafisa zenye thamani ya Tsh. 1, 237, 666, 600/=, tayari buti zimekabidhiwa kwa Jeshi hilo na hivi sasa kiwanda kinamalizia utengenezaji wa viatu vya maafisa wa Jeshi la Polisi.

Maafisa Masoko wa Kiwanda cha viatu Karanga Moshi wakivipanga viatu vya kiraia aina mbalimbali vinavyotengenezwa katika kiwanda hicho kama inavyoonekana katika picha.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akipata maelezo ya kitaalam juu ya utengenezaji wa Buti za Jeshi kutoka kwa Mtaalam wa utengenezaji viatu wa Jeshi la Magereza
(Picha zote na Jeshi la Magereza).

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI NA CGP KASIKE WATEMBELEA KIWANDA CHA SAMANI CHA JESHI LA MAGEREZA CHA ARUSHA KILICHOTEKETEA KWA MOTO


Na Lucas Mboje, Arusha
KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya  Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike leo wametembelea Kiwanda cha Samani cha Arusha, mali ya Jeshi la Magereza ili kujionea athari mbalimbali iliyosababishwa na ajali ya moto iliyotokea juzi Novemba 16, 2018.
Akizungumza eneo la tukio Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu amesema kuwa ni vyema taasisi mbalimbali nchini pamoja na wananchi wakachukua tahadhali za majanga ya moto ili kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza kufuatia majanga hayo.
Amesema kuwa Wizara yake itaendelea kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji vifaa vya kisasa ili liweze kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza.
Aidha, Katibu Mkuu huyo, Meja Jenerali Kingu amelitaka Jeshi la Magereza kuhakikisha kuwa linafanya jitihada za haraka za kurejesha shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho ikiwemo kufanyia matengenezo baadhi  ya mashine zilizoteketezwa na moto.
Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amevishukru vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha sambamba na wananchi waliojitokeza kusaidia katika uzimaji wa moto huo ambao umeunguza sehemu ya kiwanda hicho.
“Nawashukru sana Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Arusha, Jeshi la Polisi pamoja na wananchi kwa kazi kubwa waliyoifanya siku ya tukio kwani niliarifiwa kuwa moto ulikuwa mkubwa lakini tunashukuru Mungu hatimaye uzimaji ulifanikiwa pamoja na hasara iliyojitokeza”. Alisema Jenerali Kasike.
Akizungumzia chanzo cha moto huo na hasara iliyojitokeza, Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme ambayo ilisababisha kuteketea kwa baadhi ya mashine za kiwanda hicho pamoja na uharibu wa nyaraka mbalimbali za ofisi katika jengo la utawala.
Wakati huo huo, Kamishna Jenerali Phaustine Kasike ameunda Kamati maalum ya Maafisa watano kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza ambayo itachunguza chanzo cha moto huo pamoja na kuwasilisha taarifa kamili ya hasara iliyojitokeza. Tume hiyo itaongozwa na Kamishna wa Fedha na Mipango wa Jeshi hilo, Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana.
Kiwanda cha samani cha Magereza Arusha kilimikishwa rasmi kwa Jeshi la Magereza mwaka 1973 baada ya Azimio la Arusha mwaka 1967 ambapo tangu kipindi hicho kiwanda hicho kinajishughulisha na utengenezaji wa samani mbalimbali za ofisi na samani za majumbani. Pia kiwanda hiki hutumika kuwafundisha na kuwarekebisha wafungwa ili wamalizapo vifungo vyao waweze kujitegemea kupitia ujuzi waliojifunza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akiwasili Novemba 17, 2018 katika Kiwanda cha samani cha Magereza Arusha kukagua sehemu mbalimbali ambazo moto umeteketeza sehemu ya kiwanda hicho. Kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.

Mkuu wa Magereza Mkoa huo, ACP Anderson Kamtiaro akisoma taarifa ya janga la moto mbele ya Katibu Mkuu Mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu aliwasili kiwandani kujionea uhabribu mbalimbali uliojitokeza.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu Mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu kuhusu hatua mbalimbali ambazo amezichukua ikiwemo kuunda kamati maalum ya watu watano ambayo itachunguza tukio la moto katika kiwanda hicho.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike (wa pili toka kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia kwake), wakiangalia moja ya mashine mbalimbali ambazo zimeteketezwa na moto katika kiwanda cha Samani cha Magereza Arusha. Chanzo cha moto huo inasemekana ni hitilafu ya umeme ndani ya kiwanda hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo mbalimbali kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati). Kulia ni Kamishna wa Fedha na Mipango, Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana ambaye ni Kiongozi wa Kamati Maalum ya kuchunguza tukio hilo.

Jengo la kiwanda cha samani cha Magereza Arusha ambalo limeteketea kwa moto.

Muonekano wa baadhi ya mashine pamoja na vifaa mbalimbali na nyaraka nyinginezo za ofisi zilizoungua kufuatia janga la moto.

Samani mbalimbali zinazotengenezwa katika kiwanda cha samani cha Magereza Arusha kama inavyoonekana katika picha zikiwa tayari kwenda sokoni(Picha na Jeshi la Magereza).

Friday, November 16, 2018

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA AKUTANA NA RC NJOMBE KABLA YA KUHITIMISHA ZIARA YAKE TAREHE 15/11/2018

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike  alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi, Novemba 15, 2018.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka akitoa taarifa fupi ya Mkoa wake alipotembelewa na Mkuu wa Jeshi la Magereza Ofsini kwake.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike akielezea malengo ya ziara yake ya kikazi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe alipotembelea Ofisi za Mkoa huo.


Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP. Phaustine Kasike akiagana na baadhi ya askari wa Gereza Njombe baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Njombe.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe. Wa pili toka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Bw. Erick Shitindi ( Picha na Jeshi la Magereza).