Banner

Banner

Tuesday, June 23, 2020

MAFUNZO YA UHAMASISHAJI WA WAELIMISHAJI WA MTANDAO WA WANAWAKE KATIKA JESHI LA MAGEREZA NCHINI YAFUNGULIWA MKONI MOROGORO.



Na Shani Mhando, Morogoro

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jinsia katika Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Wazee na Watoto Bi.Mboni amefurahishwa kuanzishwa   kwa mtandao wa wanawake katika jeshi a magereza nchini
akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya  mtandao huo, uliofanyika katika ukumbi wa Umwema Mkoani Morogoro,Bi Mboni amesema, hii ni hatua nzuri sana yakupongezwa kwa Jeshi la Magereza kuhakikisha wanawake  katika Nyanja zote wanatumia fursa mbalimbali zilizopo na zitakazojitokeza ndani ya Jeshi na Nje ya Jeshi ili kujipatia mafanikio.
aliongeza kuwa msingi wa kuwepo kwa mitandao ya wanawake ni nchini ni kuwawezesha na kuwajengea uwezo  wanawake katika Nyanja za kiuchumi,mafunzo,ajira,uongozi na maamuzi ili kuweza kutimiza majukumu yao bila kubaguliwa jinsia zao.
“Ni matarajio yangu kuwa kuanzishwa kwa mtandao huu Jeshi la magereza litazingatia miongozo na kanuni mbalimbali zilizotolewa na serikali kuhakikisha katika maeneo yote yenye changamoto za usawa wa kijinsia mwanamke awezeshwe ili aweze kukabilina nazo,”alisema Bi Monica
Aidha Bi Mboni amewaasa washiriki wa mafunzo kuzingatia yote watakayofundishwa katika mafunzo hayo ili wakawe wawakilishi wazuri kwa askari wote wa kike katika Jeshi la Magereza ili kuwajengea uwezo,kukuza uelewa na kuwaunganisha waweze kufanya kazi kw ufanisi zaidi.
“Jukumu mlilopewa na Jeshi la Magereza la uelimshaji ni jukumu muhimu sana katika ustawi wa mtandao wa wanawake ndani ya Jeshi la Magereza, ninahakika,mafunzo mtakayoyapata yatawaongezea uwezo wa kutekeleza jukumu hili muhimu na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya mtando ndani Jeshi,”alisema Bi Mboni
kwa upande wa Mkuu wa dawati la Jinsia Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Bertha Joseph Minde amesema kuanzishwa kwa mtandao wa wanawake magereza kumewawezesha wanawake  Kushika nafasi za juu za uongozi katika Jeshi kama kamishna mmoja,kamshna msaidizi mwandamizi mmoja na makamishn wasaidizi 6 ingawa bado kuna upungufu mkubwa wa kinamama katika nafasi za juu za uongozi.
naye msemaji wa Jeshi la Magereza Mrakibu mwandamizi Amina kavirondo amemuomba Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo Bi  Mboni  kuwashika mkono mtandao wa wanawake Magereza ili kuweza kufikia malengo waliyokusudia
Aidha kamishna msaidizi mwandamizi wa mkoa wa morogoro (RPO)  Ismail T.Mlawa aliwapongeza wanawake wa Jeshi la Magereza kwa kuanzisha mtandao wa wanawake ambapo utawawezesha kupambania haki zao
 mtandao wa wanawake katika Jeshi la magereza ulianzishwa rasmi tarehe7 Desemba,2018 baada ya mkutano wa SADC uliofanyika Dec.2011 nchini Birchhood Johanesburg Africa ya Kusini ambapo katika kikao hicho wazo la mtandao wa wanawake lilirasimishwa na kuwekewa mikakati(the idea of women network consolidation and road map drawn)


Monday, June 1, 2020

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA SULEIMAN MZEE AKABIDHI MALORI MATATU KATIKA SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA MAGEREZA(SHIMA), LEO JIJINI DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(Kushoto) akikabidhi funguo za malori mapya kwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza, SACP. Chacha Bina leo Juni 1, 2020 katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akijaribu kuliwasha moja ya lori kabla ya kukabidhi malori mapya matatu kwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza, SACP. Chacha Bina(hayupo pichani) leo Juni 1, 2020 katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma.

Muonekano wa malori mapya matatu yaliyokabidhiwa kwa ajili ya shughuli za Kikosi ujenzi cha Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza, leo Juni 1, 2020 katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(wa pili toka kulia) akifanya mahojiano mafupi  na wanahabari mara baada ya makabidhiano ya malori ya Shirika la Uzalishaji mali la Magereza leo Juni 1, 2020 katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma                            (Picha zote na Jeshi la Magereza).

Tuesday, May 19, 2020

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AKUTANA NA MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA WALIOHAMISHIWA MAKAO MAKUU YA JESHI HILO DODOMA HIVI KARIBUNI

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akizungumza katika kikao kazi na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wamehamishiwa hivi karibuni Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma. Kikao hicho kimefanyika leo Mei 19, 2020 kwa lengo la kupeana mikakati mbalimbali ya kazi sambamba na maelekezo ya utekelezaji wa mageuzi yanaendelea ndani ya Jeshi hilo.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(hayupo pichani)katika kikao kazi kilichofanyika leo Mei 19, 2020 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(meza kuu) akiwa na Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP. Mzee Nyamka(kushoto) wakifuatilia kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kilichofanyika leo Mei 19, 2020, Jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jeshi la Magereza, SACP. Boyd Mwambingu akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee mara baada ya kikao kazi na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wamehamishiwa hivi karibuni Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma(Picha zote na Jeshi la Magereza).