Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza(CGP), John Casmir Minja akimvisha
cheo cha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Afisa Mwandamizi kutoka Makao
Makuu ya Jeshi la Magereza, Jeremiah Katungu katika hafla ya
uvishaji vyeo kwa Maafisa waliopandishwa vyeo ngazi mbalimbali(jana)
Machi 20, 2015 katika Viwanja ya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga,
Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja
akikagua Gadi Maalum ya Heshima iliyoandaliwa na Maafisa wa Jeshi la
Magereza katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa waliopandishwa vyeo
ngazi mbalimbali(jana) Machi 20, 2015 katika Viwanja vya Chuo cha
Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
Bendi ya Jeshi la Magereza ikipita mbele ya Mgeni rasmi Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) kutoa heshima
baada ya zoezi la uvishaji vyeo Maafisa 77 wa vyeo mbalimbali kukamilika
Maafisa wa Jeshi la Magereza Nchini pamoja na Wageni Waalikwa
wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) katika hafla ya
zoezi la uvishaji vyeo kwa Maafisa 77 wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir
Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wanawake vyeo
mbalimbali(waliosimama nyuma) baada ya zoezi la uvishaji vyeo hivyo Chuo
cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam(wa pili kushoto) ni
Kamishna Huduma za Urekebishaji, Injinia Dionice Chamulesile(wa pili
kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa
kwanza kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Kamishna
Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy.
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi
la Magereza.