Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakikata vitambaa
vya nguo kabla ya kuanza kushona nguo za Wafungwa Magerezani. Wafungwa
hao hujifunza Stadi mbalimbali za ujuzi ambazo huwasaidia kujipatia
kipato mara tu wanapomaliza kifungo chao.
Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakiendelea na
ushonaji wa nguo za aina mbalimbali kama wanavyoonekana katika picha.
Jeshi la Magereza nchini linatekeleza ipasavyo jukumu lake la
Urekebishaji kwa kuwapatia ujuzi wa fani mbalimbali Wafungwa wanapokuwa
wakitumikia vifungo vyao Magerezani.
Mkuu wa Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ismail Mlawa akiongea na Wanahabari(hawapo pichani).
Aina za nguo mbalimbali ambazo tayari zimeshonwa kwa Ustadi Mkubwa na
Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam. Gereza Kuu Ukonga Dar es
Salaam limejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kwa kutekeleza ipasavyo
Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa kwa Vitendo.
(Picha zote
na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).