Marehemu Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Aneth Laurent Balibusha
Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa kwanza kulia), Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Ally Lufunga (wa pili) na Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga (wa tatu kulia) wakibadilisha mawazo nyumbani kwa marehemu eneo la Segerea, Dar es salaam.
Mwili wa Marehemu Kamanda Aneth ukibebwa kuingizwa kwenye gari maalum kwa ajili ya kupelekwa Kanisani
Mwili wa Marehemu SACP Aneth ukiwasili katika viwanja vya Kanisa Katoliki Jimbo la Segerea kwa ajili ya kuombewa kabla ya kupelekwa Makaburini.
Makamanda wakiusindikiza Mwili wa Marehemu Altareni kwa ajili ya kuombewa.
Baadhi ya Wanafamilia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Marehemu Kamanda Aneth wakiwa Kanisani wakifuatilia Misa Takatifu.
Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa kwanza kulia) Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh.Ally Rufunga (aliyevaa miwani) na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakhim Maswi (wa tatu kulia) wakifuatilia Misa ya kumuombea Marehemu Kamanda Aneth Balibusha.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wa Jeshi la Magereza wakifuatilia Misa Takatifu ya kumuombea Marehemu Kamanda Aneth.
Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa katika ibada maalum ya kumuombea Marehemu. Kutoka kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Dkt. Juma Malewa, Kamishna wa Fedha na Utawala Gaston Sanga, RPO-Mwanza ACP Gorea, RPO-Morogoro SACP Dkt.Katto na RPO-Arusha SACP Nkubasi
Paroko Msaidizi wa Parokia ya Segerea Padre Josephat Mmbaga akiubariki mwili wa marehemu Kamanda Aneth Balibusha.
Paroko Msaidizi wa Parokia ya Segerea Padre Josephat Mmbaga akinyunyuzia maji ya Baraka Mwili wa Marehemu.
Naibu Kamishna wa Magereza Edith Malya akitoa salamu za Jeshi la Magereza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza kwa ndugu na jamaa waliohudhuria Misa Takatifu kanisani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Ally Rufunga akitoa salamu kwa niamba ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akitoa salamu za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa niamba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Kasim Mkodo kutoka Shinyanga akitoa salamu kwa niaba wa watumishi wa Magereza Mkoani Shinyanga.
Naibu Kamishna wa Polisi DCP Nyamuhanga akitoa salamu za Jeshi la Polisi.
Kamishna Mstaafu wa Huduma za Urekebishaji wa Magereza Mama Aziza Sally akitoa salamu kwa niamba ya Wastaafu wa Jeshi la Magereza lakini pia akiwa mtu aliyefanya kazi kwa muda mrefu na marehemu.
Kamishna Mkuu Mstaafu, Afande Nicas Banzi akitoa heshima zake za mwisho kwa Mwili wa Marehemu.
Kamishna Jenerali Mstaafu, Afande Augustino Nanyaro akitoa salamu zake za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliye pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mh. Ally Rufunga, Kamishna Jenerali John Minja na Eliakhim Maswi wakitoa heshima zao za Mwisho.
Mfanyakazi wa Jeshi la Mgereza, Ndugu Magret Achwari akilia kwa uchungu wakati wa kuaga mwili wa Marehemu.
Binti ya Marehemu Kamanda Aneth Bulisha akilia kwa majonzi makubwa wakati wa kumuaga mama yake.
Baada ya Misa takatifu ya kumuombea marehemu Msafara wa ndugu jamaa na marafiki ukielekea Makaburini.
Mwili wa Marehemu Kamanda Aneth ukiwasili Makaburi ya Segerea tayari kwa mazishi.
Mwili wa Marehemu SACP Aneth ukishushwa kaburini
Paroko Msaidizi wa kanisa Katoliki Jimbo la Segerea Padri Josephat Mmbaga akibariki Kaburi la Marehemu Kamanda Aneth baada ya mwili kuingizwa kaburini.
Watoto wa Marehemu Aneth wakiweka udongo kwenye kaburi kama ishara ya kumuaga mama yao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mbaraka Abdulwakil akiweka udongo kaburini.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja akiweka udongo kwenye kaburi.Wajukuu wa marehemu wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi
Katibu wa mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mbaraka Abdulwakil akiweka shada la maua kwenye kaburi.
Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja akiweka shada la maua kwenye kaburi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Ally Rufunga akiweka shada la maua kwenye kaburi.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Shinyanga akiweka shada la maua kwenye kaburi.
Kaburi la Marehemu Kamanda Aneth Bulisha likiwa limepambwa kwa mashada ya maua yaliyowekwa na ndugu, jamaa na marafiki.
Picha zifuatazo ni Gadi maalum ya Mazishi ya Jeshi la Magereza ikitoa heshima za mwisho mbele ya Kaburi la Marehemu Kamanda Aneth Balibusha.
Na ASP Deodatus Kazinja-Makao Makuu ya Magereza
Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Anneth Balibusha Laurent umeagwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Segerea na kuzikwa katika makaburi ya Segerea Jijini Dar es Salaam jana tarehe 06 Agosti, 2015.
Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Anneth Balibusha Laurent umeagwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Segerea na kuzikwa katika makaburi ya Segerea Jijini Dar es Salaam jana tarehe 06 Agosti, 2015.
SACP
Anneth aliugua ghafla tarehe 29 Julai, 2015 Mkoani Shinyanga na
kulazwa katika hospatali ya Mkoa huo lakini hali yake iliendelea
kubadilika hivyo ikawalazimu kupelekwa katika hospitali ya Rufaa
Bungando Mkoani Mwanza kwa matibabu zaidi ambapo jioni ya tarehe 30
Julai, 2015 alifariki dunia.
Akitoa
salaam za Jeshi la Magereza katika msiba huo, Naibu Kamishna wa
Magereza (DCP) Edith Malya kwa niamba ya Kamishna Jenerali wa Magereza
alisema Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla limempoteza mtu muhimu
aliyekuwa na sifa za pekee katika utendaji kazi wake lakini pia
limempoteza katika umri wake mdogo.
Alitoa
pole kwa familia, watumishi wa Jeshi la Magereza, Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Shinyanga na kwa wote walioguswa na msiba huo. Pia
aliitolea mwito familia ya marehemu kuwa wavumilifu katika kipindi hiki
kigumu lakini pia kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana na familia
hiyo kwa hali zote.
Aidha
alisema kuwa Marehemu Anneth alikuwa miongoni mwa wanawake wachache
wenye wadhifa wa Ukuu wa Magereza wa Mikoa hapa nchini ambapo jumla yao
wako walikuwa wane tu na hivi sasa wamebaki watatu.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Uslama wa Mkoa huo Ally Nassro Lufunga alisema Kamati yake imempoteza
mtu muhimu sana kwani alikuwa ni kiungo katika shughuli zao mkoani
lakini pia marehemu alikuwa ameleta mwamko mpya katika vikundi vya akina
mama na akiwa kiongozi wa vikundi vya mazoezi nyakati za jioni baada ya
kazi. RC Lufunga aliongozana na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama katika
kumzika mjumbe mwenzao.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa niaba ya
Katibu Mkuu alisema Wizara imempoteza mtendaji makini, kwamba wao kama
wizara walimtazama Marehemu Aneth kwa kuzingatia umri, elimu , jinsia
yake na cheo alichokuwa nacho kama mtu ambaye angekuja kusaidia huko
mbeleni katika ule mpango wa kurithishana madaraka. “sisi kiutumishi
pale wizarani ni pigo kubwa hatuna jinsi ni mipango ya Mungu itatubidi
kujipanga upya, pole nyote” Alihitimisha
Marehemu
Anneth Balibusha Laurent alizaliwa mwaka 1965 katika Kijiji cha Kibwera
kata ya Kihanga Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Marehemu alijunga na
Jeshi la Magereza tarehe 01 Septemba, 1994 akiwa ni Mhitimu wa Shahada
ya Kwanza ya Sanaa katika Uchumi na Mipango katika Chuo Kikuu cha Dar
es salaam (UDSM)
SACP
Anneth tangu kuajiriwa kwake amekuwa Afisa Mipango Makao Makuu ya
Magereza hadi Octoba 2013 alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Magereza Mkoani
Shinyanga.