Banner

Banner

Friday, October 14, 2016

TAMASHA LA MICHEZO GEREZA KUU UKONGA DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Global Publshers akisalimia wafungwa (hawapo pichani) mara alipowasili gerezani Ukonga katika Tamasha la Kuadhimisha Siku ya Nyerere.(Nyerere Day) leo tarehe 14, 10, 2016 jijini Dar es salaam.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitia saini kitabu kitabu cha wageni gerezani Ukonga katika Tamasha la Michezo wakati wa kuadhimisha Nyerere Day.Kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Stephen Mwaisabila, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Thom Nyanduga, Mkurugenzi wa Global Publishers Erick Shigongo na Abdalah Mrisho ambaye ni meneja wa Global Publshers.
Baadhi ya Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia kwa magunia wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016
Mmoja wa Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia na yai katika kijiti wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016
Sehemu ya Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia mita 100 wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016
Baadhi ya Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kuvuta kamba wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulienda kwa wlio kushoto
Baadhi ya Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kushikana mieleka wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016
Mkurugenzi wa Global Publishers Bw.Erick Shigongo (mgeni rasmi) akisalimiana na wachezaji kabla ya mchuano mkali nawakuvutia wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulienda kwa wenye sare Nyekundu kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoshana nguvu ya 2-2 katika muda wa kawaida
Mkurugenzi wa Global Publishers Bw.Erick Shigongo (mgeni rasmi) akisalimiana na wachezaji kabla ya mchuano mkali nawakuvutia wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulienda kwa wenye sare Nyekundu kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoshana nguvu ya 2-2 katika muda wa kawaida

Sehemu ya zawadi zilizoletwa na wageni gerezani wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani humo  tarehe 14.10.2016
Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Magereza na wageni mbalimbali wakishiriki chakula cha mchana pamoja na wafungwa (hawapo pichani) gerezani Ukonga wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani humo  tarehe 14.10.2016
Baadhi ya wachezaji wa timu iliyoibuka mshindi wakishangilia baada ya kupachika bao la kusawazisha katika dakika mbili za mwisho na kufanya mchezo kuwa 2-2 na kisha kuingia katika mikwaju ya penati zilizowa ushindi wachezaji wenye uzi mwekundu wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere nchini lililofanyika ndani ya gereza la Ukonga jijini Dar es salaam tarehe 14.10.2016
Kepteni wa Timu iliyoshinda Johnson Nguza (Papii Kocha) akibeba kombe kwa niaba ya timu yake baada ya kulipokea toka kwa Mgeni Rasmi Erick Shigongo wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dar es salaam,  tarehe 14.10.2016
Johnson Nguza aka Papii Kocha akitumbuiza kwa pamoja na wanamuziki wa Twanga Pepeta wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dar es salaam, tarehe 14.10.2016
Picha ya pamoja ya Timu iliyoibuka washindi wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi ulipatikana kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoshana  nguvu ya 2-2 katika muda wa kawaida.

Picha zote na Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza


Na ASP Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza
Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Kampuni ya Global Publishers limefanya Tamasha la michezo mbalimbali kwa wafungwa wa gereza hilo.

Akiongea katika Tamasha hilo Mkurugenzi wa Global Publishers aliyekuwa pia mgeni rasmi Bwana Erick Shigongo amewaambia wafungwa kuwa dhimra ya ujio wao gereza ni katika kuonesha kuwathamini, kuwahurumia na kuwatia moyo kwamba kuwa kwao gerezani siyo kwamba wametengwa na dunia.

Bwana Shigongo aliwatia moyo wafungwa hao kuwa hawatakiwi kukata tamaa na bado wanayo nafasi ya kubadilika na kuwa raia wema. “Kila mwanadamu anaowajibu wa kubadili maisha yake, Mwalimu Nyerere tunayemuadhimisha leo alizaliwa kama mimi na wewe na kutengeneza maisha yake na leo tunamkubuka kwanini wewe ushindwe?”

Aliongeza “ najua wengi wenu mko hapa mkiwa mmeitwa majina mengi kwakuwa mmehukumiwa, hizini hukumu za wanadamu, mnaouwezo wa kuandika kurasa mpya katika maisha yenu na siku mkitoka duniani waseme mtu mwema ameondoka. Siku moja inatosha kubadili maisha yako, kila siku andika ukurasa mpya wa maisha yako na Mungu atakuongoza alisisitiza Shigongo.

Wadau wengine walioungana na Global Publishers katika tukio hilo ni pamoja na Tume ya Haki za Binadamu Nchini ikiongozwa na mwenyekiti wake Thom Nyanduga na ndugu Rajab Maranda (aliyewahi kuwa mfungwa gereza Ukonga) ambao kwa pamoja walileta zawadi mbalimbali kwa wafungwa hao ikiwemo vifaa vya, sabuni,soda kikombe ambacho kilitolewa kwa timu iliyofanya vizuri katika mpira wa miguu.

Katika Tamasha hilo wafungwa walishiriki michezo ya kukimbia katika magunia, kukimbia na yai katika kijiti, mbio za mita 100 vijana kwa wazee, mita 400 kupokezana vijiti, kuvuta kamba, mieleka, mpira wa miguu, mashairi, kuonesha vipaji vya uchekeshaji, kuimba kwa mtindo kufokafoka, ngoma za jadi  na burudani kwa kushirikiana na baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Twanga pepeta.