Banner

Banner

Tuesday, July 11, 2017

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MUZIKI WA BRASS BAND YA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana alipowasili kwenye hafla ya  kufunga mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017(kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokea salaam ya heshima kutoka kwa gwaride maalum katika hafla fupi ya kufunga mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua gwaride maalum katika hafla fupi ya ya kufunga mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua Gadi ya wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza wakipita mbele ya jukwaa kwa heshima katika hafla ya kufunga rasmi mafunzo hayo kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa wamesimama kwa heshima kabla ya Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kupita mbele ya jukwaa kwa heshima katika hafla ya kufunga rasmi mafunzo hayo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) akiwa katika jukwaa akifuatilia kwa makini maonesho mbalimbali ya wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Naibu Kamishna wa Magereza Gideon Nkana.
Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza wakionesha onesho maalum la umbo la Mwenge wa Uhuru kama inavyoonekana kaika picha.
Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza wakitoka uwanjani mara baada ya kuonesha maonesho mbalimbali katika hafla fupi ya kufunga rasmi mafunzo hayo. Jumla ya Askari 90 wa Jeshi Magereza wamehitimu mafunzo hayo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wanawake wa  mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza. Walioketi wa pili toka kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga, (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaa, Naibu Kamishna wa Magereza Augustine Mboje, (wa tatu toka kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana, (wa pili toka kulia) ni Boharia Mkuu wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mafunzo Jeshini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Charles Novart.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).