Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akiwa kwenye gari maalum pamoja na Wastaafu wengine wa Jeshi la Magereza wakipita katikati ya Gwaride likiwa katika umbo la OMEGA ikiwa ni ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wao Jeshini. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 21, 2017.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwapungia mikono Wastaafu wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 21, 2017.
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akiwa kwenye gari maalum pamoja na Wastaafu wengine wa Jeshi la Magereza wakiwapungia mikono Wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 21, 2017.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza wakifuatilia tukio la kuagwa wastafu hao kama inavyoonekana katika picha.
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Magereza, Augustine Mboje alipowasili katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam.
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo.
Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi la Magereza likipita mbele ya wastaafu wa Jeshi la Magereza kwa mwendo wa haraka.
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akiwa jukwaa kuu wakati Gwaride likipita mbele kwa heshima.
Kamishna wa Fedha na Uatwala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga akisalimiana na Mnadhimu Msaidizi wa Jeshi la Magereza .Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Deogratis Lwanga (wa pili kulia) katika hafla ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo.
Kamishna wa Fedha na Uatwala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga (katikati) akifuatilia matukio ya kuagwa wastaafu wa Magereza, kulia ni Mnadhimu Msaidizi wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Deogratis Lwanga na wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Mlasani Kimaro.
Wastaafu wa Jeshi la Magereza walioagwa leo katika viwanja vya chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga DSM, kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Marcel Lori, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza George Kiria na Kamishna Msaidizi wa Magereza Erasmus Kundy.
Wastaafu wa Jeshi la Magereza (waliosimama nyuma) katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Magereza waliohudhuria hafla ya kuagwa kwao leo tarehe 21 Julai, 2017. Waliokaa katikati ni Kamishna wa Fedha na Utawala Gaston Sanga, wa kwanza kushoto ni Naibu Kamishna Tusekile Mwaisabila, Naibu Kamishna Uwesu Ngarama na kutoka kulia ni Naibu Kamishna Augustine Mboje na Naibu Kamishna Gedion Nkana.
(PICHA ZOTE na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Makao Makuu ya Magereza)