Banner

Banner

Friday, August 11, 2017

BURIANI MSTAAFU SACP OMARI MTIGA

Kamishna Mkuu Mstaafu wa Jeshi la Magereza, Kamanda Simon A. Mwanguku akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu.
Kamishna Mstaafu wa Huduma za Urekebishaji, Kamanda Deonis Chamulesile akimpokea Kamishna Mkuu mstaafu, Kamanda Alhaj Jumanne  Mangara aliyeambata na Naibu Kamishna  Mstaafu Green E. Mwaibako.
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Jeshi la Magereza, Kamanda Alhaj Jumanne  Mangara akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu.
Kamishna mstaafu wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza,Kamanda Deonis Chamulesile akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Magereza,aliyemwakilisha Kamishna Jenerali wa Magereza, mama Tusikile Mwaisabila, akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu.
 
Naibu Kamishna wa Magereza ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam,Augustino Mboje akiweka saini kitabu cha maombolezo.
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Green E.Mwaibako akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,ambaye ni Mnadhimu wa Jeshi, Deogratius Lwanga, akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani, Boyd P. Mwambingu, akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo.
Mwili wa Marehemu Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu wa Magereza Omari Mtiga ukiwasili nyumbani kwake Segerea.
Mke wa Marehemu Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu wa Magereza Omari Mtiga akiwa na wanae,wakiomba dua kwenye jeneza lenye mwili wa marehemu.
Mama wadogo na shangazi wa marehemu wakiomba dua mbele ya mwili wa marehemu Omari Mtiga.
Paredi maalum la Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Magereza likitoa heshima ya saluti mbele ya mwili wa marehemu.
Naibu Kamishna Mstaafu, John Nyoka akitoa salamu za maombolezo kwa wafiwa na waombolezaji kwenye msiba.
 Naibu Kamishna Tusikile Mwaisabila akitoa salamu kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza.
Naibu Kamishna Tusikile Mwaisabila akitoa rambirambi kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza kwa motto mkubwa wa Marehemu.
 Sehemu ya umati wa waombolezaji waliohudhuria msiba huo nyumbani kwa marehemu Segerea.
Waombolezaji wakipata chakula cha mchana kabla ya kwenda kumzika Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu wa Magereza Omari Mtiga.
Sehemu ya waombolezaji wakina mama  wakiwa na majonzi kwenye msiba huo huko Segerea nyumbani kwa marehemu.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu wa Magereza, Dk. Rajabu Mbiro(wan ne toka kulia) akiwa na Mkuu wa Gereza la Keko, Kamishna Msaidizi Abdalah Kiangi na makamanda wengine, wakizungumza mawili matatu kwenye msiba.
Makamishna Wakuu wastaafu,pamoja na makamnda wengine wakipita kwenye jeneza la marehemu kutoa heshima zao za mwisho.
Viongozi wa dini ya kiislam na baadhi ya waumini wa dini hiyo wakimsalia marehemu na kumuombea dua kwa Mwenyezi Mungu.
Paredi maalum la Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Jeshi la Magereza likitoa heshima ya saluti mbele ya mwili wa marehemu kabla ya kuupeleka kwenye kaburi.
Mwili wa Marehemu Kamishna Msaidizi Mwandamizi msaafu wa Magereza Omari Mtiga ukipelekwa kwenye sehemu ya kaburi lililoandaliwa kwa ajili ya mazishi hayo.
Shughuli za kumzika Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu Omari Mtiga zikiendelea makaburini.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro , Afande Ramadhan Nyamka akiweka udongo juu ya kaburi.
Paredi maalum lililoanda kwa mazishi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi msaafu wa Magereza ,Marehemu Omari Mtiga, liktoa heshima ya mwisho ya kijeshi.
Sehemu ya kikosi cha paredi maalum la mazishi kikitoa heshima ya marehemu,kamanda Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu wa Magereza Omari Mtiga, kwa kulipua risasi baridi hewani.
Sehemu ya Makamanda na waombolezaji waliohudhuria makaburini wakitoa heshima zao za mwisho baada ya kumzika kamanda Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu wa Magereza Omari Mtiga.



Kamishna Msaidizi wa Mwandamizi wa Magereza (SACP) Mstaafu  Mtiga Hussein Omari aagwa na kuziwa rasmi katika makaburi ya Kijitonyama Jijini Dar es salaam.

SACP Mtiga Omari alifariki tarehe 07. 08. 2017 katika Hosiptali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Marehemu SACP Mtiga alizaliwa tarehe 25.09.1956 katika kijiji cha Chumbi Kata ya Rusembe Tarafa ya Muhoro wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.

Alijiunga na Jeshi la Magereza mwaka 1979 akitokea Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alilojiunga nalo kwa mujibu wa sheria baada ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita (VI) katika shule ya sekondari ya wavulana Tabora (Tabora Boy’s)

Marehemu Mtiga alipata mafunzo ya ndani na nje ya kwa ngazi na nyakati tofauti ikiwa ni pamoja na Mafunzo ya Uongozi Dara la Pili na la Juu kutoka Chuo cha Maafisa  wa Magereza Ukonga (kwa sasa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Stashahada ya Uandishi wa Habari kutoka TSJ na Stashahada ya Uhusiano wa Kimataifa katika chuo cha Diplomasia Kurasini.

Mafunzo mengine ni Intelligence Security kutoka chuo cha Galilee nchini Israel na mafunzo mafupi kama vile Correctional Intelligence Management,Diplomatic Security Services nakadhalika.

SACP Mtiga ndani ya Jeshi la Magereza alifanya kazi katika vituo tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na Singida, Iringa,Uyui Tabora,Tarime na Musoma Mara na Makao Makuu kwa nyakati tofauti. Marehemu Mtiga nakumbukwa zaidi akiwa Mkuu wa Kitengo cha Intelijensia na Operesheni, Habari na Msemaji wa Jeshi la Magereza.

Marehemu alistaafu kazi rasmi mwezi 07.2016 akiwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Kagera (RPO). Ameacha na watoto watano.Wakiume watatu na wakike 2.

Kamishna Jenerali wa Magereza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE.