Friday, July 12, 2019

ZAIDI YA WAFUNGWA 640 WAMENUFAIKA NA MPANGO WA BODI YA PAROLE NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU


                      


 
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole akitoa taarifa fupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto) afungue rasmi Kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Julai 12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga,  Jijini Dar es Salaam.


           Baadhi ya Wajumbe Sekretarieti wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao hicho.


Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(hayupo pichani) akifungua kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole.

      Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(meza kuu) akiongoza Kikao cha 41 cha Bodi hiyo.

Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakifuatilia majadiliano ya wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole leo Julai 12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Jeshi la Magereza).