Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Dkt Ayubu
Rioba, leo tarehe 22,February,2021 amefanya ziara katika Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza yaliyoko Msalato Jijini Dodoma.
Akizungunza muda mfupi baada ya kuwasili ofisini hapo Rioba amesema,
madhumuni ya ziara hiyo ni kujifunza namna Jeshi la Magereza
limefanikiwa kujenga Makao yake Makuu kwa muda mfupi na kwa gharama
nafuu huku akisisitiza kuwa kilichofanywa na Jeshi hilo kinafaa
kuigwa.
‘‘ Hakika ziara yangu hii katika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
imenifanya kujifunza na kunipa mwanga zaidi wa namna ya kujipanga
kwani hata sisi TBC tunao mpango wa kujenga ofisi zetu za shirika
hapa Dodoma. Pia nashauri taasisi nyingine hazina budi kuja kujifunza
mahali hapa.’’ Amesema mkurugenzi huyo.
Awali akimpokea mkurugenzi mkuu wa TBC kwa niaba ya Kamishna Jenerali
wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Jeremiah Katungu amesema kuwa
amefurahi kwa ujio wake hivyo awe huru kujifunza na kuuliza pale
anapohitaji ufafanuzi.
Aidha Naibu Kamishna wa Magereza Jeremiah Katungu Katungu amesema,
mafanikio ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza yametokana na
mpango kabambe wa Kamishna Jenerali wa Magereza Meja Jenerali Suleiman
Mzee.
‘‘Kimsingi tunamshukuru Kamishna Jenerali wa Magereza kwa juhudi
alizozionyesha mpaka kufanikisha ujenzi wa ofisi hizi kwa muda
mfupi.’’
Pia Katungu amesema kuwa rasilimali zilizotumika kukamilisha ujenzi
huu ni za ndani tu kwani waliotumika ni maafisa na askari pamoja na
wafungwa.
Aidha amesema kuwa ujenzi huo ulianza mwezi wa tano mwaka jana hadi
kufikia mwezi Disemba mwaka jana ulikuwa umekamilika kwa kiasi kikubwa
na gharama ya ujenzi huo uligharimi kiasi cha milioni 900 taslimu.
Riyoba akiangalia akiangalia eneo la Makao Makuu Ya Magereza alipo
fanya ziara yake akiongozana na Naibu Kamishna Wa magereza Jeremia
Katungu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Justine Kaziulaya na
Mandarasi wa mradi wa jengo La Makao Makuu ya Jeshi Mkaguzi wa
Magereza Belela
akiangalia Ramani ja majengo ya makao makuu ya jeshi la Magereza alipo
tembelea makao makuu hayo
Mkurugenzi wa TBC akiangalia Bustani ya maua ya Makao makuu ya
Jeshi la Magereza
akiangalia baadhi ya ofisi akiongozana na Naibu kamishna wa Jeshi la
Magereza Jeremiah Katungu.