Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Februari 14, 2025 alifanya ziara Makao Makuu ya Jeshi la Magereza na kuzindua Mabasi Saba ya kubebea Mahabusu kwenda na kurudi Mahakamani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabasi hayo Mhe. Bashungwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri na kubwa anayo endelea kuifanya ya kuboresha Jeshi la Magere
za kwa kulipatia vifaa na vitendea kazi mbalimbali ikiwemo mabasi tuliyo yazindua na kutoa wito wa kuyatunza magari hayo ili yadumu na kutoa huduma iliyokusudiwa.
za kwa kulipatia vifaa na vitendea kazi mbalimbali ikiwemo mabasi tuliyo yazindua na kutoa wito wa kuyatunza magari hayo ili yadumu na kutoa huduma iliyokusudiwa.
"Nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambayo anaendelea kuifanya yakuboresha Jeshi letu la Magereza, kuliwezesha Jeshi letu la Magereza kuwa na vifaa na vitendea kazi kama ambavyo tumeshuhudia uzinduzi wa mabasi haya ambayo yanaenda kuboresha huduma kwa ndugu zetu wafungwa" alisema Mhe. Bashungwa
Aidha, Mhe. Bashungwa amelipongeza Jeshi la Magereza nchini kwa kutekeleza kikamilifu jukumu la kuwapa ujuzi wafungwa ikiwemo ufundi stadi na kuuendeleza ujuzi wa wafungwa wanaoingia nao, huku akieleza mkakati uliopo wa kuzindua program maalum kwa kushirikiana na VETA ili kutoa vyeti kwa wafungwa baada ya kupata ujuzi Gerezani.
Katika hatua nyingine Mhe. Bashungwa amempongeza CGP. Katungu kwa kusimamia agizo la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuachana na matumizi ya kuni na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia katika Magereza yote hapa nchini.