TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Katika kuboresha utendaji kazi ndani
ya Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Martin Kasike
amefanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi
kwa kuwateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa Tanzania
Bara(RPOs) 19 wapya na saba (7) kuwabakiza katika nyadhifa zao.
Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali Kasike ameteuwa na
kuthibitisha maafisa sita (6) kuwa Wakuu wa Vyuo vya Magereza na kuwabadilisha maafisa wengine watatu (3)
katika vitengo muhimu ndani ya Jeshi hilo.
Aidha, Kamishna Jenerali Kasike katika
mabadiliko hayo kwa mara ya kwanza
amewateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa
katika mikoa ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita ambayo ilikuwa haina
uongozi wa kimagereza katika ngazi ya mikoa hiyo.
Katika mabadiliko hayo ni pamoja na
aliyekuwa RPO (DSM) SACP. Hamis Nkubasi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya
Magereza kitengo cha Ujenzi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP. Julius
Ntambala, SACP. Salum Hussein RPO (Dodoma) amebakia katika kituo chake na
aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kiwira SACP. Luhende Makwaia anakwenda kuwa RPO (Mbeya)
na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Mathias Mkama na aliyekuwa RPO (Mbeya) SACP.
Kijida Mwakingi amehamishiwa Makao Makuu, Kitengo cha TEHAMA.
Aliyekuwa RPO (Mtwara) SACP. Ismail
Mlawa amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Mipango na nafasi yake
kuchukuliwa na ACP. Varisanga Msuya aliyekuwa Kaimu Bohari Mkuu wa Jeshi ambapo
nafasi yake inachukuliwa na ACP. Robert Masali ambaye anakuwa Boharia Mkuu wa
Jeshi la Magereza. Aliyekuwa RPO (Mwanza) SACP. Athuman Kitiku amehamishiwa
Makao Makuu ya Magereza sehemu ya Utumishi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP.
Hamza Hamza aliyekuwa RPO Tabora.
Aidha, ACP. Joseph Mkude anakuwa RPO
(Tabora) na aliyekuwa RPO (Kagera) SACP.
Boyd Mwambingu amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Utawala na nafasi yake
inachukuliwa na ACP. Rymond Mwampashe. Aliyekuwa RPO (Lindi) SACP. Rajabu
Bakari amehamishiwa Makao Makuu Kitengo
cha Mawasiliano na Usafirishaji na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Josephine
Semwenda.
Aliyekuwa RPO (Rukwa) SACP. Benno
Hunja amehamishiwa Makao Makuu sehemu ya Kilimo, Mifugo na Mazingira na nafasi
yake inachukuliwa na ACP. Jail Mwamgunda
na aliyekuwa RPO (Kilimanjaro) SACP. Hassan Mkwiche amehamishiwa Makao Makuu kuwa
Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe na nafasi yake kuchukuliwa na ACP.
Rajab Igongi. Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe ACP. Wilson
Rugamba anakuwa RPO (Shinyanga).
Pia, Aliyekuwa RPO (Morogoro) SACP. Mzee
Nyamka amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Takwimu na
nafasi yake inachukuliwa na ACP. Stylvester Mrema. Aliyekuwa Kaimu RPO (Mara)
ACP. Benezeth Bisibe amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mdhibiti wa Fedha (FC) na
nafasi yake inachukuliwa na ACP. Hospitius Adrian. Mkuu wa Mkuu wa Chuo KPF
ACP. Lazaro Nyanga anabakia katika nafasi hiyo, ACP. Anthony Sogoseye anabakia
kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani. Aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa chuo
Ruanda SSP. Enock Mwanguku anakuwa Mkuu wa Chuo hicho.
Aidha, waliokuwa Kaimu RPOs, Vyuo na
maeneo mengine ambao sasa wamethibitishwa ni kama ifuatavyo:- ACP. Hasseid
Mkwanda (Iringa), ACP. Anderson Kamtearo (Arusha), ACP. Emmanuel Lwinga
(Tanga), ACP. Masudi Kimolo (Manyara), ACP. Joel Matani (Mkuu wa Chuo cha Taaluma
ya Urekebishaji), ACP. Rehema Ezekiel (Pwani), ACP. Msepwa Omary (Singida), na
SP. Ally Uwesu (Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza).
Walioteuliwa kuwa RPOs katika mikoa
mipya ni ACP. Alexander Mmassy (Katavi), ACP. Lyzecky Mwaseba (Songwe), ACP.
Festo Ng’umbi (Njombe), ACP. Robert Rumanyika (Geita) na ACP. Andulile
Mwasampeta (Simiyu). Wakati huo huo ACP. Alexander Nyefwe anakuwa RPO (Ruvuma)
na ACP. Leonard Burushi anakuwa RPO (Kigoma) kufuatia waliokuwa RPO katika
mikoa hiyo kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria.
Maafisa wengine waandamizi walioko
Makao Makuu ambao wamepangiwa majukumu mengine ni SACP. Bertha Minde anakuwa
Mkuu wa Kitengo cha Parole na SACP. Chacha Jackson ambaye anakuwa Mkuu wa Kitengo
cha Huduma za Mahabusu.
Kwa mujibu wa Kamishna Jenerali
Kasike Maafisa wote waliohamishiwa Makao Makuu wanatakiwa kuripoti Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma.
Imesainiwa
na; Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Deodatus Kazinja – Ofisa Habari,
Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza,
DAR ES
SALAAM,
07 Novemba,
2018.