Bofya hapa kupakua tangazo la ajira
Monday, September 27, 2021
Thursday, March 11, 2021
WAFUNGWA, MAHABUSU KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA ILIYOBORESHWA (CHF).
DODOMA. Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Meja Jenerali Suleimani Mzee Leo Tarehe 11 Machi 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Dkt. Francis Lutalala, ambaye ni Mratibu wa Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF) Jijini Dodoma kwa lengo la kuona uwezekano wa kuboresha afya ya Watumishi wa Jeshi hilo pamoja na Wafungwa na Mahabusu waliopo Magerezani.
Monday, February 22, 2021
MKURUGENZI MKUU WA TBC DR. RYOBA AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Dkt Ayubu
Rioba, leo tarehe 22,February,2021 amefanya ziara katika Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza yaliyoko Msalato Jijini Dodoma.
Akizungunza muda mfupi baada ya kuwasili ofisini hapo Rioba amesema,
madhumuni ya ziara hiyo ni kujifunza namna Jeshi la Magereza
limefanikiwa kujenga Makao yake Makuu kwa muda mfupi na kwa gharama
nafuu huku akisisitiza kuwa kilichofanywa na Jeshi hilo kinafaa
kuigwa.
‘‘ Hakika ziara yangu hii katika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
imenifanya kujifunza na kunipa mwanga zaidi wa namna ya kujipanga
kwani hata sisi TBC tunao mpango wa kujenga ofisi zetu za shirika
hapa Dodoma. Pia nashauri taasisi nyingine hazina budi kuja kujifunza
mahali hapa.’’ Amesema mkurugenzi huyo.
Awali akimpokea mkurugenzi mkuu wa TBC kwa niaba ya Kamishna Jenerali
wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Jeremiah Katungu amesema kuwa
amefurahi kwa ujio wake hivyo awe huru kujifunza na kuuliza pale
anapohitaji ufafanuzi.
Aidha Naibu Kamishna wa Magereza Jeremiah Katungu Katungu amesema,
mafanikio ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza yametokana na
mpango kabambe wa Kamishna Jenerali wa Magereza Meja Jenerali Suleiman
Mzee.
‘‘Kimsingi tunamshukuru Kamishna Jenerali wa Magereza kwa juhudi
alizozionyesha mpaka kufanikisha ujenzi wa ofisi hizi kwa muda
mfupi.’’
Pia Katungu amesema kuwa rasilimali zilizotumika kukamilisha ujenzi
huu ni za ndani tu kwani waliotumika ni maafisa na askari pamoja na
wafungwa.
Aidha amesema kuwa ujenzi huo ulianza mwezi wa tano mwaka jana hadi
kufikia mwezi Disemba mwaka jana ulikuwa umekamilika kwa kiasi kikubwa
na gharama ya ujenzi huo uligharimi kiasi cha milioni 900 taslimu.
Riyoba akiangalia akiangalia eneo la Makao Makuu Ya Magereza alipo
fanya ziara yake akiongozana na Naibu Kamishna Wa magereza Jeremia
Katungu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Justine Kaziulaya na
Mandarasi wa mradi wa jengo La Makao Makuu ya Jeshi Mkaguzi wa
Magereza Belela

akiangalia Ramani ja majengo ya makao makuu ya jeshi la Magereza alipo
tembelea makao makuu hayo

Mkurugenzi wa TBC akiangalia Bustani ya maua ya Makao makuu ya
Jeshi la Magereza
akiangalia baadhi ya ofisi akiongozana na Naibu kamishna wa Jeshi la
Magereza Jeremiah Katungu.
Friday, February 19, 2021
Thursday, February 4, 2021
RAIS MAGUFULI AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA SULEIMAN MZEE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt, John Pombe Magufuli (wa tatu toka kushoto) akizindua nyumba 24 zilizopo katika viwanja vya Gereza Isanga Jijini Dodoma leo tarehe 4 Februari,2021.
Injinia wa Mradi wa Kiwanda cha samani kilichopo Msalato, Mrakibu Bonaza Malata(wa pili kulia) akitoa maelezo mafupi ya ujenzi wa kiwanda hicho kwa Rais Magufuli.
Wednesday, January 20, 2021
TANZIA: NAIBU KAMISHNA WA MAGEREZA JULIUS SANG'UDI AFARIKI DUNIA JIJINI DODOMA.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Jeshi la Magereza)
TANZIA
Kamishna Jenerali wa Jeshi Magereza Mej. Jen Suleiman M. Mzee anasikitika kutangaza kifo cha Naibu Kamishna wa Magereza Julius Mayenga Sang’udi kilichotokea Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini Dodoma leo tarehe 20 Januari, 2021.
Aidha anatoa pole kwa Familia ya Marehemu, Watumishi wote wa Jeshi la Magereza Nchini, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaendelea kuratibu taratibu za Mazishi nyumbani kwake Kisasa nyumba 300, Dodoma.
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa Ijumaa tarehe 22 Januari,2021 na Mazishi yatafanyika Mkoani Simiyu Kijiji cha Ikulilo – Mwandete Jumamosi tarehe 23 Januari,2021.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amen.
Imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Magereza,
Kitengo cha Habari na Mawasiliano ya Umma,
Dodoma.
Saturday, January 16, 2021
MAGEREZA WAOKOA BILIONI 11 ZA CHAKULA CHA WAFUNGWA.
Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Magereza nchini limeokoa jumla ya Shilingi Bilioni 11, ikiwa
ni gharama ya chakula cha wafungwa tangu lianze kujitegemea kwa
chakula ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya
kulitaka jeshi hilo litumie nguvu kazi ya wafungwa ilionao kuzalisha
chakula.
Akizungumza leo katika ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,iliyofanyika katika Makao Makuu Mapya ya Jeshi hilo ,Msalato
jijini Dodoma, Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee amesema
walikuwa wanatumia Shilingi Bilioni Moja kila mwezi kulipa wazabuni wa
chakula waliokuwa wanaliuzia chakula jeshi hilo.
“Sasa hivi tunajitegemea asilimia kubwa kwa chakula, Serikali kabla ya
mwezi wa tatu mwaka jana kila mwezi kulikua kuna deni la Bilioni Moja,
lakini baada ya mwezi huo wa tatu sasa tunaokoa kiasi hicho cha fedha
shilingi bilioni moja na mpaka sasa tuna miezi kumi na moja
tunajilisha wenyewe kupitia shirika la magereza” alisema CGP Mzee
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo
alilipongeza Jeshi la Magereza kwa kutekeleza vyema agizo la Rais
Magufuli ikiwa sambamba na ujengaji wa kiwanda kikubwa cha samani
ambapo mpaka kukamilika kwake kitagharimu shilingi Bilioni
1,101,743,123/=
“Niwapongeze kwa hatua mbalimbali za maendeleo ambazo zingine
nimeshuhudia mwenyewe,lakini kubwa kuweza kujitegemea kwa chakula cha
wafungwa hali iliyopelekea kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho
kinabaki humu humu ndani na mnakitumia kwa shughuli zingine za
maendeleo hongereni sana” alisema Naibu Waziri Chilo