Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akifungua
Kikao Maalum cha Wadau kutoka nje ya Magereza(hawapo pichani) cha
kujadili rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa
chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani. Kikao hicho kimefanyika leo
Desemba 8, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es
Salaam.
Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Beatus
Kundy(aliyesimama) akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza
wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa
waliopo Magerezani. Jeshi la Magereza limeandaa rasimu hiyo ili
kuipunguzia Serikali gharama za kuwalisha wafungwa waliopo magerezani.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini
uwasilishaji wa Andiko hilo(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Huduma za
Urekebishaji, Eng. Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa
Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Hashim
Kimmwe akitoa mchango wake wakati wa kujadili rasimu ya Mpango wa Jeshi
la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo
Magerezani.
Wataalam wa Jeshi la Magereza walioshiriki kikamilifu katika maandalizi
ya Andiko la Mpango wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula kwa
kushirikiana na Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wakifuatilia majadiliano ya rasimu hiyo.