Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.
John Mngodo akihubia Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza
lililofanyika leo Desemba 15, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa
Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali hapa nchini
wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja
akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la
Magereza lililofanyika leo Desemba 15, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la
Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Maafisa Wandamizi wa
Jeshi la Magereza kutoka Mikoa yote Tanzania Bara, Makao Makuu ya Jeshi hilo,
Wakuu wa Vyuo vya Magereza wakifuatilia majadiliano katika Baraza hilo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la
Magereza wakiwa wameshikana mikono huku wakiimba wimbo Maalum wa Mshikamano
Daima “SOLIDARITY FOREVER”.
Mgeni rasmi Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. John Mngodo akiwa katika
picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza (walisimama). Wa Pili kushoto ni Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) ni Kamishna
wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa
Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) ni Katibu wa
Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza, Haikamen Mshida.
(Picha zote na Lucas mboje wa Jeshi la Magereza).
Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
JESHI la Magereza limeaswa kuwa na matumizi mazuri ya fedha za umma ambayo
ni pamoja na kuokoa fedha ambazo zilitengwa kwa matumizi ambayo siyo ya muhimu
sana na fedha hizo kupelekwa katika mambo muhimu zaidi.
Akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Jeshi hilo, Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. John Mngodo alisema kwa
kufanya hivyo Jeshi hilo litakuwa limeunga mkono kauli ya Rais John Magufuli
ambapo Rais amekuwa akisisitiza watumishi wa umma kuokoa fedha za Serikali
katika mambo ambayo hayana ulazima.
"Tuzingatie makusanyo ya fedha za Serikali sambamba na kuokoa fedha katika
mambo yasiyokuwa ya lazima na kupeleka fedha hizo katika mambo ya muhimu zaidi"
Alisema Mngodo.
Mngodo amewataka pia watumishi hao wa Jeshi la Magereza kuzingatia nidhamu ya
matumizi ya fedha na utunzaji wa mali za Serikali.
Aidha aliwasisitiza watumishi hao kuzingatia mapambano dhidi ya Rushwa mahala
pa kazi kwa kuepuka matendo ya utoaji na upokeaji rushwa kwa kuzingatia
kauli ya Rais Magufuli kuwa “Tanzania bila ufisadi inawezekana” badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza
tija mahala pa kazi.
Mngodo katika hotuba yake hiyo aliwataka pia watumishi wa Jeshi hilo waliokuwa
kwenye Baraza hilo kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wanapodai maslahi
yao.
"Natumia fursa hii kuwataka kila mmoja wenu aliyopo hapa kubeba jukumu la
kuhakikisha kuwa maadili ya nidhamu katika utendaji kazi kuwa kama chachu ya
kuongeza ufanisi inazingatiwa kila siku," alisema Mngodo.
Mngodo alisema katika kuleta maendeleo ni muhimu kuwashirikisha wafanyakazi kwa
njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabaraza ya wafanyakazi ili kuweka mikakati
ya kuimarisha utendaji kazi na kutatua kero zinazowakabili.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti
wa Baraza hilo ambaye ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John Minja alisema
majadiliano ya Kikao hicho yataleta chachu na kuimarisha hali ya watumishi na
utendaji kazi katika Jeshi hilo.
‘’Naamini uwepo wenu hapa utakuwa ni chachu katika majadiliano ambao
utasaidia kuimarisha hali za watumishi na utendaji kazi katika Jeshi letu la
Magereza” alisema Minja.
Katika Kikao hicho kama ilivyo katika mabaraza ya wafanyakazi, hupokea taarifa
za utekelezaji wa Bajeti katika kipindi cha Mwaka 2015/2016 kunaanzia Julai
hadi Septemba Mwaka huu ambapo watajadili na kutoa mapendekezo