JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
W1ZARA YA MAMBO YA NDAN1 YA NCH1
(Jeshi la Magereza)
W1ZARA YA MAMBO YA NDAN1 YA NCH1
(Jeshi la Magereza)
Anwani ya Simu :" MAGEREZA" Simu namba: (+255) - 022 : 2110314-6 Fax: (+255)-022: 2113737 Email: cgp@prisons.go.tz UnapoJibu tafadhali taja: |
|
Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza, S.L.P. 9190, DAR ES SALAAM. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 16 Desemba 2015 saa 3:00 asubuhi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Mbarak Abdulwakil atafungua rasmi Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara utakaofanyika katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ndio Kikao cha juu kabisa Jeshini ambacho huwahusisha Wakuu wa Magereza wa Mikoa, Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu na Wakuu wa Vyuo vya Magereza. Kauli mbiu ya Mkutano huu ni utendaji kazi wenye tija, uadilifu na weledi kazini.
Madhumuni ya Mkutano huu wa kila mwaka ni kutathmini kwa pamoja utendaji wa Jeshi la Magereza katika maeneo yake yote na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo, kurekebisha dosari zilizojitokeza na kujiwekea malengo ya kuboresha utendaji wa kazi kwa ujumla katika mwaka unaofuata.
Mada kuu ya Mkutano wa Mwaka huu itatolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza ambapo mada hiyo imezingatia Kauli mbiu ya sasa ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Maamuzi na mikakati mbalimbali itakayotolewa na Mkutano huu itakuwa na umuhimu wa pekee katika kuandaa na kutoa miongozo mbalimbali ya utendaji katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hili.
Vyombo vya Habari mnakaribishwa kwenye ufunguzi wa Mkutano huo tarehe 16 Desemba, 2015 saa 3:00 asubuhi na pia katika ufungaji siku hiyo saa 9:30 alasiri.
Imetolewa na kusainiwa na;
John C. Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
14 Desemba, 2015.