Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Katungu, Oktoba 03, 2024 amekutana na Watendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Magereza (SHIMA) wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Omary Msepwa, kwaajili kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji wa Shirika hilo ili liweze kuleta tija zaidi katika Uzalishaji.